Mkurugenzi wa Mashtka nchini Biswalo Mganga akizungumza wakati wa ufunguzi wa jengo la ofisi ya taifa ya mastaka wilaya ya Kahama ambapo amesisistiza juu ya suala la ushirikiano kati ya ofisi yake na mamlaka zingine wanazofanya kazi kwa pamoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Nchini (DPP)
Biswalo Mganga amewafutia Mashtaka washitakiwa 147 katika Mkoa wa Shinyanga ambao walikuwa wakisubiri kesi zao kutajwa Mahakamani
na kuwataka kuwa raia wema katika maeneo wanayoishi sambamba na kutojihusisha
na vitendo vya uhalifu.
Akizungumza mapema Septemba 3,20202 Mjini Kahama katika
Hafla maalumu ya uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ya Wilaya hiyo Biswalo
amesema wamezingatia vigezo vikuu viwili vinavyotakiwa na kwa mujibu wa sheria ambavyo
ni pamoja na kuzingatia Maslahi ya taifa
na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha katika mashauri hayo.
“Wengine
tumewafutia mashitaka kutokana ushahidi uliopo katika mashauri yao
kutojitosheleza ambao utawezesha kuwatia hatiani pasipo kuacha shaka
yeyote,pamoja na kuangalia maslahi ya taifa katika utendeshaji wa kesi
hizo,”alisema Mganga.
Amesema kuwa miongoni makosa
yaliyofutwa kwa mahabusu hao ni pamoja na Mauaji,kupigana,kukamatwa na gongo,na
kuingia kwa Jinai(Uvamizi wa migodi bila ya kuwa na vibali) ambayo yalikuwa
bado hayajatolewa maamuzi.
Awali akitoa Taarifa ya utendaji kazi
wa Ofisi ya Mashitaka ya Mkoa wa Shinyanga Naibu Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya
shinyanga Ramli Mbuya amesema kuwa wilaya ya Kahama yenye Halmashauri tatu za
Msalala,Ushetu na Kahama Mjini zina matukio mengi ya Uhalifu ikilinganishwa na
maeneo mengine katika mkoa huo.
“Wastani
wa Mshauri mbalimbali ya Jinai yanayofunguliwa katika ofisi yetu ya mkoa kwa
mwaka kutoka kahama ni 1300 ndio maana
tumelazimika kuongeza Mahakimu wawili ili kuhakikisha wanasikiliza mashauri
hayo kwa wakati hivyo kufunguliwa kwa ofisi hiihapa kahama ni sera ya nchi na
kitaifa ya kwamba wananchi wapate huduma mahali walipo ili kutasaidia kupunguza msongamano wa wafungwa katika
Gereza la kahama,”amesema Mbuya.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali Mkoa
wa Shinyanga Bi Magreth Ndaweka amesema kuwa awali wananchi walipaswa kusafiri
umbali wa zaidi ya kilomita 100 kuafuata huduma
hizo mjini Shinyanga hali iliyokuwa ikichangia mashauri mengi kuchelewa
kusikilizwa hivyo uanzishwaji wa ofisi ya mashtaka wilaya ya Kahama utakuwa
sehemu ya kupunguiza malalamiko na msongamno magerezani.
“hii itasaidia wananchi
kupunguza gharama za wananchi kwenda sehemu nyingine kutafuta huduma zetu hii ilikuwa inatokana na wilaya hii kuwa na halmashauri tatu za kahama
mji, Ushetu na msalala hivyo walikuwa wanapata wakati mgumu sana”
Mmoja wa wakazi wa Mji wa kahama
aliyeshuhudia kufunguliwa kwa huduma za kimashitaka katika eneo hilo Wilfred Birago ameipongeza serikali kupitia
Ofisi ya taifa ya mashitaka kwa kuona umuhimu na uhitaji wa huduma hiyo na
kuamua kuwasogezea kwani walikuwa wakiitafuta umbali mrefu hali iliyokuwa
ikichangia haki kuchelewa
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Sheria na Katiba, Amoni Mpanju amesema kuwa katika ziara waliotembelea Magereza
katika Mikoa ya Shinyanga na Geita washitakiwa wengi ni wa makosa ya mauaji
yatokanayo na Ramli chonganishi yatokanayo na migogoro ya kifamilia.
“Inasikitisha kwa karine
hii bado kunawatu wanaimani za kishirikina serikali itaendelea kuchukua hatua
kali za kisheria kwa watu watakaobainika kufanya shughuli za ramli chinganishi
sambamba na wanaotekeleza mauaji hayo,”amesema Mpanju.
Sambamba na hilo Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Sheria Mpanju amewaagiza wakurugenzi wote nchini kuhakikisha kila
wanapojenga majengo ya Umma kutenga vyumba viwili kwa ajili ya Ofisi ya Taifa
ya Mashitaka ili kurahisisha utendaji kazi na utoaji wa haki kwa wananchi.
Mwisho.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju akiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Mashitaka Wilaya ya Kahama kwa ajili y ufunguzi wa ofisi hiyo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju akisaliamiana na mkuu wa wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita Mh. Martha Mkupasi wilayani Kahama
baadhi ya wakazi wa Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wakiendeleza kusikiliza maelezo ya viongozi toka ofisi ya taifa ya Mashitaka waliohudhuria ufunguzi wa ofisi ya wilaya ya Kahama mapema septemba 3
Wajumbe wa kamati za ulinzi na Usalama toka Wilaya za Kahama,Mbogwe na Bukombe wakiwa wameketi kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa ofisi ya taifa ya Mashitika katika wilaya Kahama
Viongozi mbalimbali wa wilaya za Mbogwe na Bukombe wakiwa na Naibu Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) iswalo Mganga wakiwa wamesimama kwa maombi yaliyokuwa yakiongozwa wa dini
Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP)Biswalo Mganga akiteta jambo na Naibu katibu Mkuu wizara ya katiba na Sheria Amon Mpanju wakati wa Uzinduzi wa ofisi za mashtiaka wilaya ya Kahama.
Wananchi wa Wilaya ya Kahama wakiendelea kusikiliza viongozi mbalimbali wa serikali
Mzee Wilfred Birago akizungumza kwa niaba ya wazee wa wilaya hiyo juu ya umuhimu wa uwepo wa ofisi ya mashitka wilayani humo
Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi wanyamapori nchini William Kitedi akizungumza katika hafla hiyo ya ufunguzi wa ofisi ya taifa ya mashitaka
Naibu Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya shinyanga Ramli Mbuya akizungumzia hali ya kesi ambapo amesema kuwa wilaya ya kahama pekee upokea mashitika 900
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Bi Martha Mkupasi akieleza namna wanavyosafiri umbali mrefu kufuata huduma za kimahakama kati ya Mbogwe na Kahama pia Ushirimbo ambao ni Mzunguko wa zaidi ya kilomita 200 hali inayowapa wakati mgumu
Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza mbele ya hadhara mjini Kahama
Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka nchini Edson Makalllo akieleza namna ambavyo ifisi hiyo ya wilaya ya Kahama itakavyotumika kuendesha mashitika
Mkurugenzi wa Mashitika nchini Biswalo Mganga akifurahia jambo na watumishi aliyowateua kubaki katika ofisi hiyo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa ofisi ya mashitaka wilaya ya Kahama
jengo linalotumika kama ofisi ya mashitaka ya wilaya Kahama
Mkuu wa Mashitaka Mkoa wa Shinyanga Magreth Ndaweka akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo
Watumishi wa ofisi ya taifa ya mashitaka toka mikoa ya Shinyanga,Geita na Simiyu na Mara wakiwa katika picha ya pamoja
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na naibu katibu mkuu wa wizara ya Katiba na sheria Amoni Mpanju
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP)Biswalo Mganga akiteta Jambo na Naibu katibu Mkuu wizara ya katiba na Sheria nchini Amon Mpanju
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464