SHIRIKA lisilo la kiserikali la Israel Microsoft kutoka Irael kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), limewasaidia kwa kuwapa tiba watoto 65 wenye maradhi ya moyo nchini.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa Maendeleo ya Biashara, Microsoft 4Afrika, Gustavo Raiter, nchini Tanzania, shirika hilo limekuwa likifanya kazi kwa mifumo ya aina mbili katika utambuzi, matibabu na uponyaji wa watoto ambao walipatiwa matibabu katika taasisi ya JKCI.
“Kwa upande wa matibabu, Mradi wa ‘Save a Child’s Heart’ ( SACH) umekuwa ukituma madaktari wa upasuaji, wauguzi, anesthesia, madaktari wa kawaida na perfusionists JKCI kwa miezi kadhaa ili kutoa msaada wa tiba kwa watoto wenye uhitaji zaidi,”alisema Raiter.
Alisema SACH pia hutoa nafasi za masomo kwa wauguzi, wapasuaji, anesthesia, madaktari na perfusionists kutoka JKCI kwenda Israel kwa ajili ya masomo zaidi.
Kupitia ushirikiano huo, alieleza kuwa SACH na Kituo cha Tiba cha Wolfson walitambua kuwa, kuna fursa ya kuunda mifumo mipya ya kutumia teknolojia ili kusaidia JKCI.
Mradi wa SACH umetoa tiba dhidi maradhi ya moyo kwa watoto zaidi ya 5,000 katika mataifa 60 Afrika, Asia, Mashariki na Kati, Mashariki mwa Ulaya na Bara la Amerika.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema watalaamu wa upasuaji wa taasisi hiyo wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara na wenzao wa Israel kupata ushauri.
“Tunafurahi kuwa ushirikiano huu na SACH na Microsoft utawezesha utambuzi sahihi kwa kutumia zana mbalimbali za kidigitali na kuleta manufaa kwa watoto walio nchini kwetu. Tunaingia kwa ujasiri katika ushirikiano huu wa kimatibabu na tunatarajia kuwa mstari wa mbele kufanikisha ubunifu huu,” alisema.
"Kwa mujibu wa Ripoti ya Journal Frontiers kuhusu maradhi ya moyo, watoto takribani 500,000 Afrika huzaliwa na maradhi ya moyo kila mwaka huku idadi kubwa ikiwa ni waishio nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara.
Chanzo-Habari leo