WATU 40 WASHIKILIWA PEMBA TUKIO LA WANA CCM KUKATWA MAPANGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro

Watu zaidi ya 40 wamekamatwa na jeshi la polisi visiwani Pemba kwa kuwajeruhi baadhi ya wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wanatoka msikitini.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, akizungumza wakati wa ziara yake mkoani pwani amesema wameshakamatwa watu zaidi ya 40 na tiyari ulinzi umeimarishwa.

“Wahalifu waliokata mapanga baadhi ya wakereketwa wa CCM, wamewajeruhi walikuwa wanatoka msikitini lakini Watu zaidi ya 40 na wamekamatwa nachotaka kusema wale wanajaribu toka jana tumeimarisha sana ulinzi pale”


Aidha IGP Sirro, ameongelea kuhusiana na baadhi ya watu kudai wanaowasikiliza wataingia barabarani kwa kusema kuwa watanzania sasa hivi wanauelewa hivyo wanavyokwenda kwenye mikutano ya kampeni wanasikiliza sera na si sikuhamasishwa kuingia barabarani

“Nimekuwa nikisikia watu wengine wanasema hawa watu wote wanaonisikiliza wataingia barabarani niseme wale watu wote wanaokwenda kwenye ule mkutano wanaenda kusikiliza sera wala hawaendi kwa ajili ya kuandaliwa kuingia barabarani” amesema IGP Sirro.
CHANZO: BONGO 5
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464