Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt Wilson Mahera.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imezifanyia maamuzi rufaa 46 za wagombea Udiwani, ambapo kati ya hizo imekubali rufaa 24 na kuwarejesha katika orodha ya wagombea, na kukataa rufaa 13 za wagombea ambao hawakuteuliwa, huku pia ikikataa rufaa 9 za kupinga walioteuliwa.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt Wilson Mahera, ambapo amezitaja Kata ambazo madiwani wake wamerejeshwa katika orodha ya wagombea ambazo ni Mtwivila (Iringa Mjini), Kikilo (Kondoa), Makurumula, Hezya, Makorongoni, Bwawani, Jinjimili, Kimnyaki, Lemanyata, Mkwawa, Kisarawe II, Mbadala, Lusungo, Same, Maisaka, Makuburi, Kibada, Maore, Mpanda na rufaa tatu kutoka Kata ya Msindo (Iringa Mjini).
Dkt Mahera pia amezitaja rufaa 13 zilizokataliwa za wale wagombea ambao hawakuteuliwa kutoka katika Kata za Kawajense, Mjini Chirombola, Mabokweni, Chanika, Mwamala, Kiomboi, Mwasenkwa, Old Iramba, Magara, Arri, Chapwa, na rufaa mbili kutoka katika Kata za Kibamba.
Aidha Tume hiyo pia imekataa rufaa 9 kutoka katika Kata za Nonde, Mwagata, Mabibo, Mkimbizi, Kipanga, Nsoho, Ilemi, Bagara na Nkinga.
Idadi hiyo inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa maamuzi kufikia 113 na za wagombea 149, na Tume itaendelea kutoa matokea ya maamuzi ya rufaa zote zilizowasilishwa kila siku.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464