Msanii wa Bongofleva, Ben Pol
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Benard Paul a.k.a Benpol ameutangazia umma kubadili itikadi ya imani (Dini) kutoka kwenye Ukristo kwenda kwenye Uislam.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Benpol ame-share picha zinazomuonyesha akiwa kwenye vazi rasmi la Kiislam (Kanzu), akiwa msikitini na kuambatanisha maneno yanayosomeka "Bismillah-hir-Rahman-nir-Rahim 🙏🏾 23.10.2020"
Pia #CloudsDigital imepata nakala ya cheti cha msikiti Masjid Ma'Moor kinachoonesha taarifa za Benpol kubadili Dini na kubadilisha jina rasmi kutoka Benard na kuwa Behnam.
Nakala ya cheti kinachothibitisha Msanii Ben Pol kubadili dini