Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga (kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Mufindi katika hafla fupi iiliyofanyika Makao Makuu ya Wilaya hiyo mjini Mafinga.
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa upatikanaji wa haki baina yao bila uonevu wowote.
Akieleza hayo katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani humo, ikiwa ni lengo la kusogeza huduma karibu kwa wananchi walio wengi.
Aidha Bw. Mganga ameongeza kuwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi ni kuwa na utawala bora, kulinda haki na amani kwa kila Mtanzania na kupunguza malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi walio wengi na kuahidi kuwashughulikia wale wote ambao wanavuruga usalama wa nchi yetu.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William amepongeza jitihada hizo za kuhakikisha Ofisi hiyo inafunguliwa Wilayani hapo ambapo amesema kufunguliwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imekuwa ni faraja kubwa kwa wananchi wa Taifa letu.
Hivyo basi, anaamini wananchi wake watapata elimu ya kutosha juu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, inafanyaje kazi na kuhakikisha haki inatendeka baina ya wananchi. Na pia Mhe. Jamhuri aliwaasa wananchi wake kuitumia vizuri Ofisi hiyo na kuhakikisha kutoa ushirikiano ipasavyo.
Kwa upande wake mmoja wa waandishi waliohudhuria hafla hiyo ameishukuru Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kuwasogezea wananchi huduma hiyo kwa ukaribu zaidi na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wananchi kwani walikuwa wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Naye Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo alitoa wito kwa Wakuu wa Wilaya waendelea kujitolea Ofisi kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa Mashtaka kwani Ofisi zilizopo ni chache. "Hadi sasa tumefanikiwa kufungua jumla ya Ofisi za Wilaya 15, ukizingatia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka zinapaswa kuenea jumla ya Wilaya 139".
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo akitambulisha wageni waliohudhuria katika hafla fupi ya uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Mufindi iliyopo mjini Mafinga Leo
Baadhi ya Waalikwa wakiwepo Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini, Wananchi na Watumishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Mufindi wakifuatilia hotuba zinazotolewa katika hafla ya Uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Mufindi Iiliyofanyika Makao Makuu ya Wilaya ya Mufindi mjini Mafinga leo
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Mufindi katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wilaya ya Mufindi yaliyopo mjini Mafinga Leo