
Watoto wenye ulemavu wa akili wakifanya usafi wa mazingira
Na Shinyanga Press Club Blog
Changamoto ya baadhi ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga kuwaficha watoto wenye ulemavu wa akili baada ya kuzaliwa imeanza kupungua baada ya wadau wa maendeleo ya jamii kushirikiana na serikali kufuatilia na kufichua kaya zenye watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali waliofichwa majumbani na kuwatoa kuwapeleka shule.
Mwandishi wetu amefika katika kituo kinacholea watoto waliookolewa wakiwa wamefichwa majumbani baada ya kuzaliwa na changamoto ya ulemavu wa akili, ambapo wadau wa maendekeo ya jamii kutoka Kituo cha Brothers of Charity kinachojihusisha na malezi ya watoto hao kilichoko eneo la Majengo Mapya Kitangili mjini Shinyanga, kupitia kwa Br. Valentine Alexander wameeleza kuridhishwa na mabadiliko hayo na kuiomba jamii iendelee kuwathamini watoto hao ili nao wapate haki wanazostahili.
Kwa upande wao baadhi ya walezi wa watoto hao, wamesema kuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali wakati wa malezi ya watoto hao, ambapo wameomba msaada wa hali na mali kwa wadau na serikali.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo Kitangili, Mohamed Mlabu amethibitisha kukitambua kituo hicho na kwamba kimekuwa msaada kwa watoto wengi wenye ulemavu wa akili (mtindio wa ubongo), ambapo pia amebainisha amekuwa akishirikiana na wadau wanaokiendesha kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili watoto hao.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Emmanuel Ngabi, amekiri kuwepo kwa hali ya kufichwa watoto wanaozaliwa wakiwa na ulemavu wa akili katika baadhi ya familia mkoani shinyanga na kueleza kuwa Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali kupiga vita hali hiyo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Brothers of Charity kinachojihusisha na malezi ya watoto hao kilichoko eneo la Majengo Mapya Kitangili mjini Shinyanga, Br. Valentine Alexander

Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Emmanuel Ngabi

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo Mapya Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga, Juma Mlabu

Mlezi wa watoto hao, Vedastina Elias

Kituo cha Brothers of Charity kinacholea watoto wenye ulemavu wa akili

Watoto wenye ulemavu wa akili wakijifunza darasani

Watoto wenye ulemavu wa akili wakifanya shughuli mbalimbali za mikono

Watoto hao wakijishughulisha na kazi za mikono

Elimu ikitolewa kwa watoto hao

Watoto wenye ulemavu wa akili wakipata elimu

Watoto wakifanya usafi wa mazingira katika kituo kinachowalea cha Brothers of Charity

Wakielekezwa kazi mbalimbali za mikono