KMC FC KUMALIZIA HASIRA KESHO KWA POLISI TANZANIA

Kikosi cha timu ya KMC

Na Christina Mwagala, Dar es Salaam
Kikosi Cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kimetuma salama kwa Timu ya Polisi Tanzania kuwa wajipange kwa mchezo wa kesho kwani wanazawadi ambayo wamewaandalia.

Kesho kikosi hicho kinachonolewa na kocha mzawa Habibu Kondo kitashuka Dimbani kuwavaa Polisi Tanzania ikiwa ni wenyeji wa mchezo huo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

KMC FC imetamba kuwafunga wapinzani wao kutokana na kufanya mazoezi ya kutosha na kwamba wakotayari kwa ajili ya kuwa kata vipande vipande ili kujiweka katika nafasi nzuri ya msimu wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.

Kikosi hicho ambacho kimekuwa kikifanya vizuri katika msimu huo wa Ligi kuu Tanzania kimejipanga vizuri na kwamba hakuna mchezaji mwenye majeraha na hivyo kikotayari kupambania ushindi hapo kesho na hivyo kuibuka na pointi tatu muhimu.

"Kikosi chetu kipo vizuri, Polisi Tanzania wajiandae kwani mchezo wakesho utakwenda kuturudisha kwenye kasi ya mchezo wa kutokufungwa kila mechi, na hivyo kuwapa furaha mashabiki wetu,".

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464