Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kwamba limepokea taarifa ya kutokea vifo vya watu 12 hadi sasa vilivyotokana na athari ya mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam.
Oktoba 13, 2020 kuanzia alfajiri mvua kubwa ilianza kunyesha na kuendelea mchana kutwa ambapo ilisababisha foleni kubwa barabarani Jijini Dar es salaam na kupelekea mafuriko katika maeneo kadhaa.
Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema kuwa watu nane walikufa katika Mkoa wa Kipolisi Ilala na wa nne kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakiwemo watoto wawili wa familia moja.
“Watoto hao walifariki kwa kusombwa na maji baada ya nyumba yao iliyopo katika bonde la Kigogo kujaa maji na watoto hao kushindwa kujiokoa” Mambosasa