MAGUFULI ATINGA ARUMERU, JOSHUA NASSARI AWASIHI WANANCHI KUICHAGUA CCM



KATIKA mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni kuomba kura kwa wananchi katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Leo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amefanya mkutano katika jimbo la Arumeru mkoani Arusha katika viwanja vya Usa River.

Na miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Joshua Nassari ambaye kwa sasa ni kada wa CCM, amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumpigia kura Magufuli na kumuamini.
Yaliyojiri Kwenye Viwanja Vya USA River, Arumeru Mkoani Arusha ambako Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli amefanya Mkutano Mkubwa wa Kampeni muda mfupi uliopita. Arumeru wanasema walikosea sana na Sasa wamejifunza na hawataki tena kufanya Makosa. Watatoa kura zote Kwa CCM kwa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani siku ya Oktoba 28.
#KuraKwaMagufuli2020
#T2020JPM

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464