MAHAFALI DARASA LA SABA BUHANGIJA YAFANA, AFISA ELIMU AAHIDI KULETA WALIMU

Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye Mahafali yao iliyofanyika leo Oktoba 22, 2020 mjini Shinyanga
 
Na Marco Maduhu, Shinyanga 
Shule ya Msingi Buhangija iliyopo Manispaa ya Shinyanga, imefanya mahali ya 15 ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu Darasa la saba Septemba, 2020. 

Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2020 shuleni hapo, na kuhudhuriwa na wazazi, walimu, huku mgeni rasmi akiwa ni Afisa Elimu Taaluma Shule za Msingi Manispaa ya Shinyanga, Wingwila Kitila aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Geofrey Mwangulumbi. 

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Wingwila Kitila, amewataka wanafunzi hao pindi watakapo ingia kidato cha kwanza, wakaendeleze juhudi za kusoma kwa ajili ya maisha yao ya baadae, na siyo kwenda kucheza ambapo watajikuta wakizima ndoto zao na kuishia mitaani kuranda randa. 

“Kuhitimu elimu hii msingi ya darasa la saba siyo kwamba ndio mmemaliza masomo, bali ndio mmeuanza mwendo, mkifika huko Sekondari mkaongeze bidii za kujisomea, pamoja na kuwa na nidhamu ya hali ya juu, ili mpate kufikia ndoto zenu,” amesema Kitila. 

Katika hatua nyingine ameahidi kuitatua changamoto ya upungufu wa walimu maalum shuleni hapo, ambapo tayari wameshatuma maombi Tamisemi kuomba walimu, na wanasubili uchaguzi uishe ili ajira zitoke na kuitatua changamoto hiyo. 

Kwa upande wake Afisa Elimu Kata ya Ibinzamata ilipo shule hiyo, Mackline Shija, amewataka wazazi kuendeleza malezi bora kwa watoto wao ambao wamehitimu darasa la saba na siyo kuwa acha wakidhurura hovyo mitaani, na kujikuta wakiingia kwenye makundi mabaya na hata kuambulia mimba za utotoni. 

Akisoma risala ya wahitimu hao, Naziri Vicent amesema wamehitimu wanafunzi 110, wavulana wakiwa 54 na wasichana 56, na kubainisha changamoto ambayo wanaicha shuleni hapo ni upungufu wa walimu maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mgeni Rasmi Afisa elimu Taaaluma manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila akizungumza kwenye mahafali hao.
Afisa elimu Kata ya Ibinzamata manispaa ya Shinyanga Mackrine Shija, akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwalimu mkuu Shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya, akizungumza kwenye Mahafali hayo na kuipongeza Serikali kwa kujenga uzio kwenye mabweni ya kulea watoto wenye ualbino.
Mhitimu wa Darasa la saba Naziri Vicent akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake.
Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali ya watoto wao waliohitimu Drasa la Saba.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali ya watoto wao waliohitimu Drasa la Saba.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali ya watoto wao waliohitimu Drasa la Saba.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali ya watoto wao waliohitimu Drasa la Saba.
Walimu Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye mahafali.
Walimu Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye mahafali.
Keki ya mahafali wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija.
Mgeni Rasmi Afisa elimu Taaluma manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila akikata keki.
Mgeni Rasmi akitoa vyeti kwa wahitimu Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Buhangija.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Mgeni Rasmi, akitoa cheti cha pongezi kwa Muhitimu Naziri Vicent, aliyefanya vizuri kitaaluma Shuleni hapo kwa upande wa wavulana.
Mgeni Rasmi akitoa cheti cha pongezi kwa Mwanafunzi Amina Mhina, aliyefanya vizuri kitaaluma shuleni hapo kwa upande wa wasichana.
Wahitimu Darasa la Saba wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Burudani ikiendelea kutolewa.
Wanafunzi wanaobaki shule wakitoa burudani ya mitindo.
Wanafunzi wanaobaki shule wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Burudani ikiendelea kutolewa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464