Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa
Na Shinyanga Press Club Blog
KESHO (Jumapili) Kikosi cha timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars) kitashuka dimbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuwakaribisha majirani zao Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kupigwa saa 10 jioni.
Mgeni rasmi wa mchezo huo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jioni na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Lorietha Laurance, imethibitisha ushiriki wa Waziri Mkuu, huku Watanzania wakihamasishwa kujitokeza kuishangilia timu ya Taifa itakayoongozwa na Nahodha Mbwana Samatta.
Soma zaidi taarifa hiyo hapa chini