Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Zlatko Krmpotic
SAA kadhaa baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, Zlatko Krmpotic kufukuzwa kazi kwa kile kilichotajwa kuwa kiwango kibovu cha soka la timu hiyo kinachoonyeshwa uwanjani, raia huyo wa Yugoslavia amesema haoni sababu kwanini mkataba wake na mabingwa hao wa kihistoria umevunjwa.
Kocha Krmpotic ametoa kauli hiyo leo Oktoba 4, 2020 katika mahojiano yake na mwanahabari na mchambuzi wa soka nchini, Ali Kamwe.
Kocha huyo amedumu Yanga kwa takribani siku 37, huku akiiongoza klabu hiyo katika michezo mitano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, akishinda minne na sare moja, akiwa hajapoteza mchezo wowote. hata hivyo kandanda lisilovutia uwanjani limetajwa kama sababu ya kocha huyo kutimuliwa mitaa ya Jangwani.
Barua kutoka klabu ya Yanga ikielezea kuachana na kocha wake