Wachezaji wa Simba na Yanga wakichuana kwenye moja ya mchezo uliozikutanisha timu hizo msimu uliopita
Na Shinyanga Press Club Blog
BODI ya Ligi Tanzania (TPLB) imetangaza kuusogeza mbele mchezo namba 61 wa Ligi Kuu (VPL) wa watani wa jadi Simba na Yanga uliokuwa uchezwe Oktoba 18, 2020.
TPLB imetangaza uamuzi huo leo Oktoba 7, 2020 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, zikiwa zimebaki takribani siku 11 mchezo huo upigwe kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, huku chanzo kikitajwa kuwa ni hofu ya vikwazo vya usafiri wa kimatifa kutokana na uwepo janga la Corona.
Hata hivyo, Bodi hiyo imeupangia tarehe mpya mchezo huo, ambao sasa utachezwa Novemba 7, mwaka huu saa 11 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Pitia hapa chini taarifa hiyo kutoka Bodi ya Ligi