MEMBE AELEZA ALIVYOPANGA KUIPINDUA CCM KABLA HAJAFUKUZWA

Bernard Membe

Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe, amesema kuwa kabla hajafukuzwa na chama chake cha awali cha CCM, alikuwa anao mpango wa kukipindua chama hicho kiuongozi kwa kushirikiana na watu wengine sita na alikuwa na jumla ya wabunge 78.

Kauli hiyo ameitoa hii jana Oktoba, 19, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo pia ameeleza mustakabali wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 28 ,mwaka huu, kwa kuuaminisha umma wa Watanzania kuwa yeye ndiye mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo.

“Mimi nilikuwa CCM nikatataka kukabiliana na rais aliyepo madarakani peke yangu kumuondoa, lakini washukuru walinifukuza, tulijianda na wana CCM wenzangu, achilia mbali tulikuwa watu 6 tuliokuwa tayari kuiondoa serikali madarakani, mimi nilikuwa na wabunge 78, kwa bahati mbaya 46 wamefyekwa lakini wako CCM, 32 wamebaki hata mkininyonga siwezi kuwataja kwa sababu watatumbuliwa tu,” amesimulia Membe.

Aidha, Membe ameongeza kuwa, “Kuungana kwa vyama vya upinzani ni lazima chama tawala kipasuke ili kundi la pili lije upande wa pili ili kusaidia chama tawala kuangushwa CCM mwisho wake umefika na tunawaondoa madarakani Oktoba 28”.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464