TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi imefanya ufuatiliaji kwenye miradi yenye thamani ya Sh 1,845, 690, 295.52 katika ujenzi wa nyumba za watumishi, madarasa na maji, ambapo ukaguzi huo ulibaini mapungufu mbalimbali ikiwemo ucheleweshaji wa kukamilisha miradi, kutokamilisha ufungaji milango na miradi kutokaguliwa na wahandisi licha ya taarifa za utekelezaji wake kueleza imekamilika kwa asilimia 100.
Hayo yameelezwa na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Charles Mulebya leo Oktoba 22, 2020 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ikiwa ni ukaguzi wa kipindi cha miezi miwili Julai hadi Septemba, mwaka huu.
Soma zaidi taarifa hiyo hapa chini