NEC YAKANUSHA KURA FEKI KUKAMATWA KAWE, PANGANI NA KIGOMA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekanusha uzushi unaoenea mitandaoni ukisambazwa na baadhi ya watu wakidai uwepo wa kura feki katika baadhi ya maeneo wakati zoezi la upigaji kura za kuchagua rais, wabunge na madiwani likiendelea.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Oktoba 28, 2020, na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kufuatia tukio hilo.

“Kuna taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa kura feki kwenye majimbo ya Kawe Dar, Pangani Tanga, na Buhigwe Kigoma, taarifa za madai hayo ya jumla ambayo si rasmi na hazijathibitishwa, na hayaelezwi ni vituo vipi vinahusika na matukio hayo.

“Vivyo hivyo taarifa za madai hayo hazijawasilishwa rasmi kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, hivyo inawasihi wananchi wapuuze taarifa hizo,” Jaji Stomistocles Kaijage.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464