NKULILA AWAOMBA WANA NDEMBEZI AWAMU NYINGINE AKAMILISHE MIRADI ILIYOSALIA

Mgombea udiwani CCM Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga David Nkulila akinadi Sera kwa wananchi ili wamchague Oktoba 28 kuwa diwani wao.

Na Marco Maduhu, Shinyanga 
Mgombea udiwani wa Kata ya Ndembezi Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), David Nkulila, amewaomba wananchi wa Kata hiyo wamchague kwa awamu nyingine tena kuwa diwani wao, kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu, ili akamilishe miradi ya maendeleo ambayo aliianzisha kwenye kipindi kilichopita. 

Nkulila ametoa ahadi hizo leo kwenye mkutano wake wa kampeni eneo la Tambukaleli, wakati akinadi sera zake kwa wananchi wa Kata ya Ndembezi, kuwa wamchague tena ili aendelee kuwa letea maendeleo ikiwamo kupigania haki za wanyonge. 

Amesema wananchi wa Kata hiyo wasije wakafanya makosa siku ya uchaguzi, na kumpigia kura mgombea mwingine wa upinzani, bali wakampigie kura nyingi za ushindi ili aendelea kuwaletea maendeleo, pamoja na kukamilisha miradi mikubwa ambayo aliianzisha ukiwamo wa machinjio ya kisasa na kituo cha afya. 

“Mimi ni diwani mpenda maendeleo na nimtetezi wa haki za wanyonge, hivyo nipigieni kura nyingi za ushindi siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, pamoja na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, na mgombea Urais John Magufuli ili kwa pamoja tuwaletee maendeleo,”alisema Nkulila. 

“Katika kipindi kilichopita cha uongozi wangu kama diwani wa Kata hii, na dhani mmeshuhudia kazi ambazo nilizifanya, ikiwamo kutatua migogoro ya ardhi, na upimwaji wa viwanja, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami kutoka Kalogo hadi Bugoyi, ujenzi wa machinjio ya kisasa, kituo cha afya, na awamu ijayo tutajenga kituo cha Polisi,”aliongeza. 

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni, amewasihi wananchi hao wa Ndembezi siku hiyo ya uchaguzi, wakimaliza kumpigia kura mgombea Urais John Magufuli, Mgombea ubunge Patobas Katambi, na madiwani wote wa CCM, waondoke kwenye vituo vya kupigia kura na kusubili matokeo wakiwa nyumbani. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye mkutano huo wa Kampeni.
Mwenyekiti wa (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, (kushoto), akimnadi Mgombea udiwani Kata ya Ndembezi David Nkulila kwa wananchi wa Kata hiyo, kuwa siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, wampigie kura za ushindi.
Baadhi ya wenyeviti wa mtaa kutoka Kata ya Ndembezi, wakiwa kwenye mkutano huo wa Kampeni.
Mkutano wa kampeni ukiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464