Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli
Baada ya siku 60 za kuzunguka nchi nzima kukutana na Watanzania na Kunadi Sera na Ilani bora ya CCM, hatimaye Mgombea Urais wa CCM anahitimisha Kampeni zake Dodoma na kurudi Makao Makuu.Ni Kesho Jumatatu Oktoba 26, Dkt John Pombe Magufuli atahitimisha Kampeni zake Mkoani Dodoma. Watanzania wamesikia na wamejionea Sera nzuri zilizohubiriwa na CCM kote nchini na Sasa wako tayari kutoa kura Zote kwa CCM.