SHINYANGA KUANZISHA MAONESHO YA BIASHARA, TEKNOLOJIA YA MADINI NA VIWANDA



Na Marco Maduhu

Shinyanga.

Manispaa ya Shinyanga imepanga kuanzisha maonesho ya biashara, teknolojia ya madini na viwanda, kwa ajili ya kukuza ustawi wa shughuli za kilimo, ufugaji, viwanda, madini, ili kuunda mnyororo wa thamani ambao utakuza uchumi wa wananchi na mkoa kwa ujumla.


Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amebainisha hayo leo, kwenye kikao cha wafanyabishara na Sekta ya madini, kwa ajili ya kujadili namna ya kufanikisha maonesho hayo ambayo yatafanyika Novemba 7-14 mwaka huu katika eneo la OldShinyanga.

Amesema Shinyanga ina utajiri mkubwa wa madini, pamoja na kuwapo na uzalishaji mkubwa wa bidhaa za viwanda, na kuna wafanyabishara wengi, lakini wamekosa fursa za kutangaza biashara zao kitaifa, pamoja na kupata mtandao wa masoko ambao utawakuza na kunyanyuka kiuchumi.

“Maonyesho haya ya biashara tuliyajadili kwa muda mrefu, pamoja na kufanya tafiti mbalimbali na kujifunza kutoka kwa wenzetu, namna walivyofanikiwa kufanya maonesho yao, sababu mji wa Shinyanga sasa hivi umeshakua, ndipo tukaona na sisi mwaka huu tuanzishe maonesho ambayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka,”amesema Mwangulumbi.

“Tayari tumeshatenga eneo la hekali 50 ambalo lipo eneo la Oldshinyanga, ambapo wafanyabiashara watakuwa wakipeleka bidhaa zao kujitangaza, pamoja na kubadilishana mawazo na wenzao, na kupata mtandao wa masoko, na pia tutavutia wawekezaji kuja kuwekeza hapa Shinyanga na hatimaye mji kukua kimaendeleo,”ameongeza.

Naye mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo John Tesha, ametaja bidhaa ambazo zitakuwa zikionyeshwa kwenye maonesho hayo, kuwa ni mashine za kilimo, vyakula vya lishe, ufugaji wa wanyama, vifaa vya kufugia mifugo, uzalishaji wa mifugo, na vifaa vya famasia.  
 
Ametaja maonesho mengine kuwa ni uzalishaji wa vifungashio, ambavyo vimekuwa changamoto kubwa kwa wazalishaji wa ndani, ambapo watakutana na wenzao na kisha kubadilisha uzoefu namna wao walivyofanikiwa, na hatimaye kundokana na changamoto hiyo.

“Niwakati muafaka manispaa yetu kuwa na maonesho haya, ili kuwaleta pamoja wazalishaji wa malighafi na watengenezaji wa bidhaa na walaji wa bidhaa hizo, ambayo yatasaidia kuibua na kubaini fursa na vikwazo vilivyopo katika sekta ya uzalishaji, na kuisaidia Serikali kuja na mpango mkakati wa kuzitatua,”amesema Tesha.

“Makadirio ya awali ya bajeti ya maonesho haya ni Shilingi 137,000,000, ambapo tutajenga majukwaa, Ofisi, jengo la migahawa, vyoo na mabafu, miundombinu ya umeme, ujenzi wa maghara, pamoja na matangazo,”ameongeza.
Naye Afisa madini mkoa wa Shinyanga Mhandisi Joseph Kumburu, amepongeza uanzishwaji wa maonesho hayo, ambapo mbali na biashara, pia yatasaidia kukuza Sekta ya madini na kukaribisha wawekezaji kuja kuwekeza Shinyanga, mkoa ambao unautajiri mkubwa wa madini yakiwamo madini ya ujenzi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda ((TCCIA) Mkoani Shinyanga Kulwa Meshack, amepongeza uanzishwaji huo wa maoenesho hayo ya biashara, ambayo yatakuwa ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara kujitangaza na kupata mtandao wa masoko.

Pia alitolea mfano wazalishaji wa ngozi, ambazo kwa sasa zinaoza sababu ya kukosa soko.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye kikao hicho.

Afisa madini mkoa wa Shinyanga Mhandisi John Tesha, akizungumza kwenye kikao.

Katibu tawala msaidizi mipango na uratibu mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru, akizungumza kwenye kikao hicho.

Meneja wa Sido mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa maandalizi ya maonesho hayo ya biashara John Tesha akielezea namna maonesho hayo yatakavyofanyika.
Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda ((TCCIA) Mkoani Shinyanga Kulwa Meshack, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini Shirema Hamza Tandiko, akizungumza kwenye kikao hicho.

Wadau wakiwa kwenye kikao.

kikao kikiendelea.

kikao kikiendelea.

kikao kikiendelea.

kikao kikiendelea.

kikao kikiendelea.

Wadau wakiwa kwenye kikao.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464