Leo Oktoba 2, 2020 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije ametaja kikosi cha wachezaji 25 watakaoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Burundi utakaopigwa Oktoba 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.
Ambapo wachezaji wataanza kuripoti kambini kuanzia Oktoba 5, 2020 baada ya michezo ya mwishoni mwa wiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL).
Katika orodha hiyo, Klabu ya Simba imetoa wachezaji saba ambao ni Golikipa Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Said Ndemla, John Bocco na Mzamiru Yassin, huku Yanga SC Wakiingiza wachezaji wanne ambao ni Metacha Mnata, Bakari Mwamnyeto, Ditram Nchimbi, Feisal Salum.
Vinara wa Ligi Kuu Tanzania, Azam FC imetoa wachezaji wanne kwenye kikosi hicho ambao ni David Kisu, Brayson Sebo, Iddi Nado na Salum Abubakar.