TAKUKURU YAWABURUZA KORTINI WATUMISHI WATATU TPA TUHUMA ZA UKWEPAJI KODI, KUSABABISHA HASARA

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo

Na Shinyanga Press Club Blog
LEO Oktoba 12, 2020 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatarajia kuwafikisha mahakamani watu wanne wakiwemo waliokuwa watumishi watatu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na mfanyabaishara mmoja kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.

Katika taarifa ya taasisi hiyo iliyotolewa leo na Ofisa Uhusiano, Doreen Kapwani kwa niaba ya Mkuugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jen. John Mbungo, imesema kuwa watuhumiwa hao wanne wanakabiliwa na makosa ya rushwa, uhujumu uchumi, kuisababishia hasara ya Sh 619, 278, 260.52 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na ukwepaji kodi unaofikia jumla ya Sh 37, 837, 409.26.

Soma zaidi hapa chini taarifa kutoka TAKUKURU



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464