Mkuu wa Wilaya akizungumza na baadhi ya
wachezaji wa timu ya watumishi FC inayomikiwa na Halmasahuri ya msalala baada ya
mchezo wa mshindi wa tatu kumaliza na timu hiyo kushinda mabao 11-0 dhidi ya
timu ya bulyanhulu.
Na Neema Sawaka,Kahama
WADAU wa mchezo soka Katika Halmashauri
ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameiomba Halmashauri hiyo
kuwasaidia wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu katika shule za
sekondari kwa kupitia Michezo kwa kujenga uwanja katika wa mpira wa miguu ili kuweza
kuhimili katika kuwatafutia karo za shule.
Mratibu wa
mashindano ya kombe la Mahona,Patrick Mahona alisema wamesaidia Wanafunzi wengi
waliopo katika mazingira magumu kusoma kupitia mchezo wa mpira wa miguu kila mwaka ambapo
mpaka sasa wamewasomesha wanafunzi 15
kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Aliyasema hayo wakati wa fainali za mashindano hayo
juzi ambayo hufanyika kila mwaka katika Halmashauri ya Msalala, huku
lengo kubwa likiwa ni kusaidia watoto kuwalipia karo za shule pamoja na
mahitaji mengine waliopo katika mazingira magumu.
Mahona ambaye ni
Mtendaji wa Kata katika kata ya segese amesema kwa sasa mashindano hayo yanachezwa katika
uwanja wa shule ya msingi Segese na iwapo halmashauri itawajenga uwanja wake
hata idadi ya wanafunzi inaweza kuongezeka.
Mahona amesema mashinado
hayo kwa sasa yanatimiza miaka saba tangu yaanzishwe mwaka 2014 yakifadhiliwa na baadhi ya wadau
katika kata ya segese yakiwemo makampuni ya madini ya wachimbaji wadogowadogo
ya Mmilic Gold plant namba nne, Masangi Gold Plant, Domain Gold pamoja ba
Azan Logistc ikiwa lengo kuu ni kuinua vipaji katika kata hiyo.
Alisema kuwa
kutokana na changamoto hiyo ya ukosefu wa uwanja Uongozi wa ligi hiyo kwa
kushirikiana na kijiji husika umetafuta eneo ambalo litafaa kujengwa uwanja wa
mpira na kuiomba Halmashauri ya Msalala iwasaidie fedha za kulipia eneo hilo.
Alisema kuwa
Halmashauri ya Msalala haina eneo la uwanja wa michezo ambapo wameomba kata ya
segese iwe kituo cha michezo mbalimbali katika Halmashauri hiyo ya msalala.
Mahona alisema
kuwa katika mashinado hayo yalijumuisha timu 16 huku zikiwa katika makundi manne ambapo katika mchezo wa jana wa kutafuta
mshindi wa kwanza mpaka wa tatu timu ya
watumishi kutoka Halmashauri ya Msalala ilikuwa mshindi wa tatu bada ya
kuifunga Bulyanhulu mabao 11-0.
Mshindi wa pili alikuwa ni Young Boys ya Segese
ambayo ilipata kichapo cha mabao 7-2 dhidi ya Mguu Target,Mshindi wa kwanza
katika mashindano hayo ilikuwa timu ya Mguu Target.
Mshindi wa kwanza ilipata Kombe na seti
ya jezi na kiasi shilingi milioni moja wakati wa pili Young Boys ilipata sh
400,000pamoja na jezi huku timu ya watumishi ikipata sh 200,000.
Akifunga
mashindao hayo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha aliwataka wadau
mbalimbali wa michezo katika jamii kujitokeza kwa wingi katika kuinua vipaji na
kuongeza kuwa kama vitaendelezwa vipaji vinaweza kujipatia ajira na
kufika mbali.
Mashindao ya
Kombe la Mahona ambayo hufanyika kila mwaka yamejijengea sifa kwa kutoa baadhi ya wachezaji
akiwemo Adam Salamba ambaye yuko Namungo FC, Mnyonge Athumani aliyopo JKT,
Revocatus Malima aliyepo Gwambina FC, Samson Mdeleke Mbeya City pamoja na
Moris Mahela Gwambina FC.