PICHA: WAZIRI KABUDI ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali jana, Oktoba 14, 2020. 
Ajali hiyo ilitokea eneo la Kihonda, Manispaa ya Morogoro katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro, chanzo kikidaiwa kuwa ni dereva wa Bajaj kuchomekea mbele ya gari la waziri huyo ghafla.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464