Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga mjini (CCM), Patrobas Katambi, akinadi sera leo Oktoba 21, 2020 kwa wananchi wa kata ya Kambarage manispaa ya Shinyanga.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi, ameendelea na kampeni zake za kunadi sera kwa wananchi wa jimbo hilo, na kuahidi kuwaletea maendeleo endapo wakimchagua kuwa mbunge wao Oktoba 28 mwaka huu.
Katambi ameendelea na kampeni zake leo, ambapo alikuwa kwenye Kata ya Kambarage, huku akiwa na Mgombea udiwani wa Kata hiyo Hassani Mwendapole, pamoja na viongozi wa CCM, wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Mkadamu.
Amesema akishachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo, atahakikisha mji wa Shinyanga ana ubadilisha kimaendeleo na kukua kiuchumi, pamoja na kuboresha sekta ya afya, elimu, miundombinu ya barabara, ujenzi wa masoko ya kisasa, Standi ya mabasi, maegesho ya malori na ujenzi wa chuo kikuu.
“Naombeni wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini, siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, mnipigie kura nyingi za ushidi ili niwe mbunge wenu pamoja na madiwani wote wa CCM na Mgombea urais John Pombe Magufuli, ili tukafanye kazi kama timu moja na kuwaletea maendeleo,” amesema Katambi.
“Mimi nitakuwa mbunge wa kazi tu na siyo Porojo, hivyo ni chagueni ili muone kama sitawaletea maendeleo, mnipime kwa miaka mitano muone kazi yangu, nilikuwa mkuu wa wilaya Dodoma makao makuu ya nchi nadhani mmejionea kazi niliyoifanya ya maendeleo, hivyo hivyo nitakavyo ubadilisha mji wa Shinyanga,” ameongeza.
Pia Katambi aliahii kushughulika na watumishi wa afya ambao siyo waaminifu, wanaowaambia wagonjwa wenye kadi za bima ya afya CHFkuwa hakuna madawa, bali wakanunue kwenye maduka ya madawa kwa kutumia fedha zao mfukoni, bila ya kuwa andikia maelezo ya kwenda kupewa dawa bure kwenye maduka yanayotoa huduma hiyo ya CHF.
Katika hatua nyingine aliwataka vijana na akina mama, wajiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ili wanufaike na mikopo fedha za halmashauri asilimia 10, ambazo zinatolewa bila riba ili wapate kujiinua kiuchumi.
Naye Mgombea udiwani wa Kata ya Kambarage, Hassani Mwendapole, aliwataka wananchi wa Kata hiyo wasifanye makosa siku hiyo ya kupiga kura, ambapo wakikosea kuchagua viongozi ndiyo watakuwa wamechagua namna ya kuishi maisha yao ndani ya miaka mitano, na kuwataka wamchague ili amalizie shughuli za maendeleo ambazo alisalia kuzimalizia kipindi kilichopita.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Abubakari Mkadamu, amewataka wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini, siku ya uchaguzi Oktoba 28 wakawapigie kura za ushindi wagombea wote wa CCM, ambao ndiyo wenye kuwaletea maendeleo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Katambi akiendelea kunadi sera kwa wananchi wa Kambarage ili wamchague kuwa Mbunge wao Oktoba 28 mwaka huu.
Mgombea udiwani wa Kambarage Hassani Mwendapole akinadi sera zake kwa wananchi ili wamchangue kuwa diwani wao Oktoba 28 mwaka huu.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Mkadamu, akiomba kura kwa wananchi wa Kambarage kuwa pigia kura wagombea wote wa CCM Oktoba 28 mwaka huu.
Mgombea udiwani wa vitimaalum Shela Mshandete, akiomba kura kwa wananchi wa Kambarage kuwapigia kura wagombea wote wa CCM kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.