138 WAKIWEMO WATENDAJI WA SERIKALI WAHITIMU MAFUNZO JESHI LA AKIBA SHINYANGA, DC MBONEKO AWATAKA KUTOPIGA WATU HOVYO MITAANI

 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (aliyevaa suti nyeusi yenye rangi ya bendera ya taifa) akikagua gwaride la Jeshi la akiba katika sherehe za kuhitimishwa kwa mafunzo ya jeshi hilo leo mjini Shinyanga.

Na Marco Maduhu -Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, amehitimisha rasmi mafunzo ya Jeshi la akiba kwa vijana 138 kutoka manispaa ya Shinyanga. 

Zoezi la kuhitimisha mafunzo hayo limefanyika leo Novemba 13, 2020 katika viwanja vya mtaa wa Mabambasi Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga na kushuhudiwa na wananchi wa maeneo hayo. 

 Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo, DC Mboneko amewataka vijana hao kuwa chachu ya kudumisha amani ndani ya jamii na wasiwe chanzo cha kuvuruga amani na kuanza kupiga watu hovyo. 

"Nyie mmeshaiva mara baada ya kupata mafunzo ya Jeshi la akiba, na kuwa askari kamili, hivyo mkirudi mitaani msiwe chanzo cha uvunjifu wa amani, bali mkawe walinzi wa amani," amesema Mboneko. 

Pia amewataka wajiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali, ili wapate fedha za halmashauri na kufanya biashara mbalimbali, ambazo zitawainua kiuchumi, na kuacha kujiingiza kwenye vikundi vya uharifu, sababu wameshapata mafunzo ya kijeshi. 

Mmoja wa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la akiba, Ezra Majerenga, akisoma risala, amesema wamehitimu 138, wavulana 114, na wasichana 24. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kufunga rasmi mafunzo ya Jeshi la akiba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akionya vijana hao waliohitimu mafunzo ya Jeshi la akiba kwenda kufanya fujo mitaani na kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
Mshauri wa Jeshi la akiba wilaya ya Shinyanga Ford Mwakasege, akisoma taarifa ya mafunzo hayo ya Jeshi la akiba.
Mhitimu wa mafunzo ya Jeshi la akiba Ezra Majerenga akisoma risala kwa niaba ya wenzake.
Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga ikiwa kwenye kuhitimisha mafunzo ya Jeshi la akiba.
Wananchi wakishuhudia ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la akiba.
Wananchi wakishuhudia ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la akiba.
Vijana waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba wakisiliza nasaha kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu Jeshi la akiba wakiwa kwenye Gwaride.
Wahitimu Jeshi la akiba akila kiapo cha utii.
Wahitimu Jeshi la akiba akifurahia mara baada ya kuhitimu mafunzo yao.
Burudani zikitolewa.
Burudani zikiendelea kutolewa.
Burudani zikiendelea kutolewa.
Burudani zikiendelea kutolewa.
Wahitimu waliofanya vizuri wakipewa zawadi.
Wahitimu waliofanya vizuri wakipewa zawadi.
Wahitimu waliofanya vizuri wakipewa zawadi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (Katikati)akipiga picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wilaya, na wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la akiba. 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464