Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga jana tarehe 26 Novemba amesikiliza na kuwafutia Kesi watu 51 wakiwepo wanaume arobaini na tisa na wanawake wawili waliokuwa katika gereza la Babati mkoani Manyara. Katika zoezi hili Bw.Mganga aliongozana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Manyara, Hakimu wa Wilaya pamoja na Mawakili kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Baada ya kuwafutia Mashtaka aliwataka wakirudi uraiani kuwa raia wema na kutorudia kutenda makosa.
Aidha, aliwaeleza kwamba jukumu la Ulinzi wa nchi yetu Tanzania ni la kila mmoja wetu na hivyo kila mmoja kujitahidi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha anailinda nchi dhidi ya maovu.
Mkurugenzi wa mashtaka nchini, DPP, watatu (Kulia) Biswalo Mganga, katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Manyara, ametembelea magereza mkoani humo na kusikiliza wafungwa na mahabusu na kuwafutia kesi 51 wakiwemo wanawake 2 waliokuwa na makosa mbalimbali..