AGPAHI YASHIRIKI KONGAMANO LA AFYA DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akifungua Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Nchembe amefungua Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit) litakalojikita katika kujadili masuala mbalimbali ya afya hasa katika kipindi hiki ambacho nchi imeingia katika uchumi wa kati. 

Kongamano hilo litakalofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia leo Jumatano Novemba 25,2020 hadi Novemba 26,2020 linafanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma limekutanisha pamoja wadau wa sekta ya Afya kutoka taasisi za Umma,Mashirika ya dini na binafsi. 

Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi ni Miongoni mwa wadau wa afya wanaoshiriki katika Kongamano hilo linaloongozwa na Kauli Mbiu ya “Mafanikio ya Uchumi wa Kati Katika Kuweka Afya Bora kwa Watanzania – Transforming The Success of Middle – Income Economy Into a Healthier Nation)"

Akizungumza wakati wa kufungua Kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe amesema licha ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa na serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi lakini bado kuna baadhi ya watu wanashindwa kuvifikia vituo vya afya na kupata huduma za afya. 

Kufuatia changamoto hiyo, amewataka Wataalamu wa Sekta ya Afya nchini kuhakikisha wanafikiria namna ya utoaji huduma bora na kwa gharama nafuu ili wananchi wenye hali zote waweze kuzimudu.

“Naomba mtumie kongamano hili kujadili ni namna gani tutoe huduma bora za afya, namna gani tuboreshe vifaa, miundo mbinu katika hospitali zetu.Namna gani tufanye ili kila mtu apate huduma za fya”,amesema Prof. Mchembe. 

“Kupitia kongamano hili tujadili na kutoa mapendekezo ya namna ya kuwasaidia kupata huduma za afya watu wa hali ya chini wakiwemo wakulima ambao hawawezi kufikia huduma za afya na hawana na bima za afya. Ni vyema kuwaza vyema tunamsaidiaje mwananchi wa hali ya chini kupata huduma bora, zenye unafuu na zinazofikika kila sehemu bila kumuumiza mwananchi”,ameongeza Prof. Mchembe.

Hata hivyo amesema Wizara ya Afya itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote ili kufanikisha utoaji huduma bora na nafuu kwa wananchi na kusisitiza kuwa ni muhimu mijadala itayoendelea katika Mkutano huo kuhakikisha inapita kwenye malengo ya Wizara yakiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto, kupunguza maambukizi ya VVU, TB, Ukoma. 

Prof. Mchembe amewataka Wataalamu hao kujadili masuala ya kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanaongeza mzigo kwa Serikali kutokana na gharama za kuyatibu magonjwa hayo.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe amesema Serikali imefanya maboresho mengi katika miaka saba iliyopita na kwamba kama wasimamizi wa Sera watahakikisha maazimio yatakayotoka kwenye kikao hicho yanaingizwa kwenye mipango ya utekelezaji kwenye Hospitali zote ngazi ya Wilaya, Halmashauri na zahanati kwa utekelezaji zaidi. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akifungua Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akifungua Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akifungua Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akifungua Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi wakiwa kwenye Kongamano la Afya jijini Dodoma leo Novemba 25,2020.

Wadau wa afya wakiwa kwenye Kongamano la Afya jijini Dodoma leo Novemba 25,2020.
Wadau wa afya wakiwa kwenye kongamano.
Wadau wa afya wakiwa kwenye kongamano la afya.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe akizungumza kwenye Kongamano la Afya nchini linalofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe akizungumza kwenye Kongamano la Afya nchini linalofanyika jijini Dodoma.
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kongamano la Afya.
Wadau wa afya wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii, Peter Maduki akizungumza kwenye Kongamano la Afya.
Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii, Peter Maduki akizungumza kwenye Kongamano la Afya.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kongamano la afya.
Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akijiandaa kukabidhi vyeti kwa washiriki wa Kongamano la afya.
Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la AGPAHI, Alio Hussein ambaye ni Meneja Mradi AGPAHI mkoa wa Mara cheti cha Ushiriki wa Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit).

Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe cheti cha Ushiriki wa Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akipiga picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Afya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akipiga picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Afya.
Wafanyakazi wa AGPAHI wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe (wa tatu kulia).
Awali Meneja Mradi AGPAHI mkoa wa Mara (kushoto) , Alio Hussein akiwasili katika Kongamano la Afya.
Wafanyakazi wa AGPAHI wakiwa kwenye kongamano la afya.
Wafanyakazi wa AGPAHI wakiwa kwenye kongamano la afya.
Wadau wa afya wakiwa kwenye kongamano la afya.
Wadau wakiwa kwenye kongamano la afya

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464