TGNP YATOA MAFUNZO YA JINSIA KWA WANAJAMII, WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI MSALALA

 

Mwanaharakati wa masuala ya jinsia na haki za binadamu Gemma Akilimali akizungumza wakati wa mafunzo hayo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa mafunzo ya kubadilisha mtazamo wa kifikra kuhusu masuala ya jinsia na elimu juu ya mipango na bajeti zenye mrengo wa kijinsia kwa Wanajamii na Watendaji wa vijiji na kata za Shilela na Lunguya halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. 

Mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku sita yameanza Jumatatu Novemba 9,2020 katika ukumbi wa Mabingwa Bugarama katika halmashauri ya Msalala yanatolewa kwa kundi la watu wapatao 60, ikiwa ni pamoja na wanajamii 40 na viongozi mbalimbali wa ngazi ya vijiji, kata na halmashauri hiyo.  

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Gemma Akilimali ambaye ni Mwanaharakati wa masuala ya jinsia na haki za binadamu amesema mafunzo yaliyoandaliwa na TGNP kwa ufadhili wa UNFPA na KOICA  yatawawezesha washiriki kubadilisha mitazamo yao na ya jamii kuhusu mila zinazomkandamiza mwanamke na kumrudisha nyuma kufikia huduma muhimu za kijamii na kiuchumi.

"TGNP inaendesha mafunzo haya ya siku sita kwa wanajamii wakiwemo wanavituo vya taarifa na maarifa na viongozi wa kata na vijiji yenye lengo la kubadilisha mitazamo  ya kijamii ambayo imegubikwa na mila na desturi kandamizi zinazorudisha nyuma jitihada za maendeleo yenye usawa wa kijinsia kwenye jamii hiyo",amesema Gemma. 

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yamekuja kufuatia utafiti wa kijamii ulioendeshwa kwenye kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Msalala ambao umebainisha mila mbalimbali kandamizi kwa wanawake na watoto wa kike. 

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Gemma Akilimali ambaye ni Mwanaharakati wa masuala ya jinsia na haki za binadamu akizungumza wakati mafunzo ya kubadilisha mtazamo wa kifikra kuhusu masuala ya jinsia na elimu juu ya mipango na bajeti zenye mrengo wa kijinsia kwa Wanajamii na Watendaji wa vijiji na kata za Shilela na Lunguya halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumanne Novemba 10,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Gemma Akilimali ambaye ni Mwanaharakati wa masuala ya jinsia na haki za binadamu akizungumza wakati wa mafunzo hayo

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Magdalena George akitoa mada kuhusu masuala ya jinsia ambapo alisema nchi yoyote ama jamii yoyote ambayo inawashirikisha wanawake katika ngazi za maamuzi imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Magdalena George akitoa mada kuhusu masuala ya jinsia

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Magdalena George akitoa mada kuhusu masuala ya jinsia

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala Neema Katengesya akizungumza wakati wa mafunzo hayo

Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini

Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini

Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.

Mafunzo yakiendelea

Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini

Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini

Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464