APS YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE 400 KWA WANAFUNZI 30 SHULE ZA MSINGI, DC MBONEKO APONGEZA



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Msingi Ushirika.


Na Kadama Malunde, Shinyanga
KATIKA kuhakikisha watoto wa kike wanasitirika wawapo shuleni na kupunguza utoro wawapo kwenye hedhi, Kampuni ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS Company) inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa Taulo za kike maarufu kwa jina Kipepeo Pad imetoa msaada wa taulo za kike 400 kwa wanafunzi 30 wanaosoma katika shule ya msingi Ushirika na shule ya Sekondari Chamaguha zilizopo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.

Hafla fupi ya makabidhiano ya Taulo za kike ‘Pedi’ imefanyika leo katika shule ya Ushirika na Chamaguha na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya APS Janeth Dutu aliyeambatana na baadhi ya waliokuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa kupokea Taulo hizo za kike kutoka Kampuni ya APS, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko aliishukuru Kampuni ya APS kwa msaada huo akibainisha kuwa zitasaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi wa kike wanapokuwa katika hedhi.

"Asanteni sana APS Company kwa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi 10 wanaosoma katika shule ya msingi Ushirika na wanafunzi 20 wanaosoma katika shule ya sekondari Chamaguha watakazozitumia kwa muda wa mwaka mmoja. Hakika mmeunga mkono kwa vitendo kampeni yetu ya ‘Msitiri msichana,punguza utoro shuleni’ tuliyoianzisha hivi karibuni”,amesema Mboneko.

“Tunakushukuru ndugu yetu Janeth Dutu kupitia Kampuni yako ya APS pamoja na waliowahi kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika ambao umeambatana nao leo kuleta taulo za kike. Hii ni sadaka kubwa mmetoa”,ameongeza Mboneko.

Mkuu huyo wa wilaya ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia upatikanaji wa taulo za kike shuleni kwani bado wanafunzi wa kike wanapata changamoto akieleza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki.

Katika hatua nyingine Mboneko amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuepuka vikundi viovu na vishawishi mbalimbali vinavyoweza kukatisha ndoto zao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS), Janeth Dutu amesema lengo la kutoa taulo za kike ni kupunguza utoro shuleni kwani baadhi ya wanafunzi wa kike wamekuwa hawaendi shuleni kutokana na kukosa taulo za kike wanapokuwa katika hedhi.

Amesema kutokana na uwepo wa taulo za kike wanafunzi watahudhuria masomo yao hata kama wapo katika hedhi hivyo ufaulu wao utaongezeka.

“Ninaamini kabisa taulo zetu za kike zinazojulikana kwa jina la Kipepeo Pad ambazo zina ubora wa hali ya juu zitawasaidia wanafunzi 10 katika shule ya msingi Ushirika ambayo nilisoma lakini pia wanafunzi 20 katika shule ya sekondari Chamaguha ambapo nitaendelea kuwahudumia wanafunzi hawa kwa muda wa mwaka mmoja”,amesema Janeth.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi walionufaika na msaada huo, Elizabeth Kagongoo kutoka shule ya sekondari Chamaguha ameishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike akieleza kuwa awali walikuwa wanalazimik kutumia vitambaa na wakati mwingine baadhi yao kuwa watoro shuleni pindi wanapokuwa katika hedhi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Msingi Ushirika.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika. Kushoto ni Afisa Mtendaji Kata ya Chamaguha, Irene Mshandete. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akielezea lengo la kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Ushirika na shule ya sekondari Chamaguha kuwa ni kusaidia kupunguza utoro shuleni kwani baadhi ya wanafunzi wa kike wamekuwa hawaendi shuleni kutokana na kukosa taulo za kike wanapokuwa katika hedhi. 

Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akimkabidhi Taulo za kike Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika iliyopo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 2,2020 katika shule ya msingi Ushirika.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akionesha taulo za kike 'Kipepeo Pad' zilizotolewa na Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika iliyopo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.

Muonekano wa sehemu ya taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika na shule ya sekondari Chamaguha zilizotolewa Kampuni ya APS.

Muonekano wa sehemu ya maboksi yenye taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika na shule ya sekondari Chamaguha zilizotolewa Kampuni ya APS.

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika ambayo pia alisoma wasome kwa bidii.

Waliowahi kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika walioambatana na Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Ushirika wakiwa wamekaa. Wa kwanza kushoto ni Zubery Bundala akifuatiwa na Agnes Mambosasa, Eva Laurent na Sara Elias.

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu na Sara Elias wakipiga picha na wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika.

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu na Sara Elias wakiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu na waliowahi kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika wakipiga picha ya kumbukumbu na wanafunzi na mmoja wa walimu wa muda mrefu wa shule hiyo baada ya kutoa taulo za kike.

Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akimkabidhi Taulo za kike 'Kipepeo Pad' Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha iliyopo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 2,2020 katika shule ya Sekondari Chamaguha.

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akionesha na kuwaelezea wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari Chamaguha namna taulo za kike 'Kipepeo Pad' zilivyo bora.

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akiwaonesha wanafunzi wa shule ya Sekondari Chamaguha namna taulo za kike 'Kipepeo Pad' zilivyo bora.

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akiwaonesha wanafunzi wa shule ya Sekondari Chamaguha namna taulo za kike 'Kipepeo Pad' zilivyo bora.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Sekondari Chamaguha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Sekondari Chamaguha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Sekondari Chamaguha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.

Elizabeth Kagongoo kutoka shule ya sekondari Chamaguha akiishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike.

Afisa Elimu Sayansi Kimu na Afya Manispaa ya Shinyanga, Beatrice Mbonea akiishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike

Mkuu wa shule ya sekondari Chamaguha, Komanya Mathias Busasi akiishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike

Wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha wakionesha Taulo za kike 'Kipepeo Pad'

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko, Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Viongozi wa kata ya Chamaguha, Manispaa ya Shinyanga, walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha wakipiga picha ya kumbukumbu.

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha.

Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464