Askofu Mkuu wa EAGT Kanda ya Ziwa Magharibi aliyechaguliwa jana, Raphael Machimu
Na Shinyanga Press Club Blog
ASKOFU wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) Tambukareli mkoani Shinyanga, Raphael Machimu amechaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo (EAGT) Kanda ya Ziwa Magharibi inayojumuisha mikoa ya Kagera, Geita na Shinyanga.
Uchaguzi wa kumpata Askofu huyo ulifanyika jana Novemba 25, 2020 mjini Kahama, ambapo Askofu Machimu alichaguliwa kwa kura za Wachungaji 463 wote waliohudhuria kutoka katika Majimbo 8 ya Kanda ya Ziwa Magharibi ili aweze kuiongoza kanda hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Akitangaza matokeo hayo, Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Tanzania, Brown Abel Mwakipesile alisema Kanda ya Ziwa Magharibi ina wachungaji 714 lakini waliojitokeza kwenye zoezi hilo la uchaguzi ni 463 ambao wote walimchagua Askofu Machimu.
Askofu Mwakipesile amewataka viongozi waliochaguliwa kuhakikisha wanadumisha, amani, umoja na mshikamano katika kulijenga kanisa la Mungu
Aidha wachungaji hao walimchagua Mchungaji Zacharia Ngurume kuwa Makamu Askofu wa Kanda ya Ziwa Magharibi, Mchungaji John Okong'o kuwa Katibu wa Kanda hiyo pamoja na Mchungaji Winfrida James kuwa Mweka hazina wa kanda hiyo.
Kwa upande wake, Askofu Raphael Machimu baada ya kuchauguliwa, amewashukuru wachungaji wenzake na kuahidi kufanya kazi kwa bidii pamoja na kudumisha umoja na mshikamano kwa wachungaji na viongozi ili waweze kuendelea kuhubili na kulitangaza neno la Mungu.
Askofu Mkuu wa EAGT Tanzania, Brown Abel Mwakipesile
Askofu Mwakipesile akizungumza na wachungaji (hawapo pichani) wakati wa mchakato wa uchaguzi huo
Kamati Kuu ya Kanisa la EAGT iliyosimamia uchaguzi huo
Katibu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Leonard Mwizarubi
Kamati ya uchaguzi ikihesabu kura
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Wachungaji wakifuatilia mchakato wa uchaguzi huo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464