BAVICHA SHINYANGA WAMVAA MDEE NA WENZAKE, WATAKA WAKIOMBE RADHI CHAMA

Mwenyekiti wa Baraza la vijana (BAVICHA) Jimbo la Shinyanga mjini Samson Ng'wagi, katikati, akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni Mwenyekiti wa BAWACHA Jimbo la Shinyanga mjini Zena Gulam, na kulia ni Katibu mwenezi wa BAVICHA, Ibrahimu Isack.

                                      Na Marco Maduhu

BARAZA la vijana la Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema (BAVICHA) jimbo la Shinyanga mjini, limemtaka mwenyeki wa Baraza la wanawake Taifa (BAWACHA), Halima Mdee, pamoja na wenzake 18 wakiombe radhi chama hicho.
Mwenyekiti wa baraza hilo Samson Ngwa'gi, amebainisha hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Chadema kanda ya Serengeti.

Amesema kitendo alichokifanya Halima Mdee pamoja na wenzake 18 kukisaliti chama, na kwenda bungeni Jijini Dododoma kuapishwa kuwa wabunge vitimaalum ni kosa kubwa, na wamestahili kuadhibiwa na kamati kuu.

"Baraza la vijana jimbo la Shinyanga mjini, tunaunga mkono maamuzi yaliyotolewa na kamati kuu ya kuwavua nyazifa zao na uanachama Halima Mdee pamoja na wenzake 18," amesema Ng'wagi.

"Pia tuna waomba wafuate maagizo ambayo yametolewa na Kamati kuu dhidi yao, ya kuomba radhi ama kukata rufaa, tunataka chama chetu tuendelee kuwa imara na tusigawanyike kwa maslahi binafsi," ameongeza.

Pia amesema ndani ya chama hicho hakuna mfumo dume ambao umedaiwa kuwapo na Halima Mdee, na kueleza kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu uliopita, chama hicho ndicho kilipitisha wagombea wengi wa nafasi ya ubunge ambao ni wanawake.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la wanawake jimbo la Shinyanga mjini (BAWACHA) Zena Gulam, ameeleza kusikitishwa na kitendo ambacho amekifanya Halima Mdee, akidai kuwa ni kiongozi ambaye alikuwa akimfuata nyayo zake, lakini kwa tukio hilo limemvunja moyo.

Aidha Novemba 24 Halma Mdee pamoja na wezake 18, walikwenda Bungeni jijini Dodoma na kuapishwa kuwa wabunge vitimaalum kupitia Chadema, lakini Novemba 27 wakafukuzwa na kamati kuu ya Chama hicho, wakidaiwa kukisaliti chama, kwa madai hawakuteuliwa kuwa wabunge wa viti hivyo ndani ya chama.

Mwenyekiti wa Baraza la vijana (BAVICHA) Jimbo la Shinyanga mjini Samson Ng'wagi, katikati, akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni Mwenyekiti wa (BAWACHA) Jimbo la Shinyanga mjini Zena Gulam, na kulia ni Katibu mwenezi wa BAVICHA, Ibrahimu Isack. Mwenyekiti wa (BAWACHA) Jimbo la Shinyanga mjini Zena Gulam, akizungumza kwenye kikao hicho.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464