Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magugu, Adeltus Rweyendera amehukumiwa kifungo cha miaka 3 au kulipa faini ya Milioni 1.5 kwa kupokea rushwa ya Tsh. 150,000.
Mtuhumiwa aliomba rushwa kwa Wazazi na ndugu wa Washtakiwa watatu ambapo kila mmoja akitakiwa kutoa Tsh. 50,000 kama kishawishi cha kuwasaidia.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani humo, Hole Joseph Makungu amesema walifanya uchunguzi baada ya kupokea taarifa kisha wakamkamata na kumfikisha Mahakamani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464