HATIMILIKI 192 ZATOLEWA KWA WANANCHI VIJIJI VYA JOMU NA KASINGILI WILAYANI SHINYANGA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akimkabidhi hatimiliki Mzee Nassoro Seif.
 
Na Marco Maduhu -Shinyanga
Wananchi wa kijiji cha Jomu na Kasingili halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamepewa hatimiliki ya ardhi, ambapo zoezi la kugawa hati hizo limefanyika jana, ambalo liliongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko. 
 
Mboneko akizungumza wakati wa kukabidhi hati hizo miliki za ardhi, amesema zitasaidia wananchi kuondoa migogoro ya ardhi, pamoja na kuongeza thamani ya ardhi yao.

"Natoa wito kwa wananchi wa Shinyanga mmpime viwanja vyenu, pamoja na kupata hatimiliki, ambayo itawasaidia kuondoa migogoro, kuongeza thamani ya ardhi, ikiwamo na kukopa fedha na kuendesha maisha yenu," amesema Mboneko.

"Pia kwenye ardhi zenu hizo katika kipindi hiki cha mvua, naomba mpande miti kwa wingi ili mvua za upepo zitakapo nyesha, zisiweze kuezua mapaa ya nyumba zenu," ameongeza.

Naye Kamishina wa ardhi msaidizi mkoa wa Shinyanga, Ezekiel Kitilya, amesema katika kijiji cha Jomu wametoa hatimiliki 20, ambapo Kijiji cha Kasingili wametoa hatimiliki 172 za kimila.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya ardhi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Julius Maira, amesema zoezi hilo la upimaji ardhi na kugawa hatimiliki ni endelevu, na kubainisha mpango wa Serikali ni kuhakikisha hadi ifikapo 2025 ardhi yote ya Tanzania iwe imeshapimwa.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamepata hatimiliki akiwamo Nassoro Seif, wameipongeza Serikali kwa kuwapatia hati hizo pamoja na kusogeza huduma kuwa karibu, tofauti na zamani mpaka waende mkoani Simiyu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye zoezi la ugwaji wa hatimiliki kwa wananchi wilayani humo.

Kamishina wa ardhi msaidizi mkoani Shinyanga Ezekiel Kitilya, akizungumza kwenye zoezi la ugwaji wa hatimiliki.

Mkuu wa idara ya ardhi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Julius Maira, akitoa taarifa namna wanavyofanya kazi ya kupima aridhi pamoja na kutoa hatimiliki.

Mjane Leticia Mhoja akiishukuru Serikali kwa kumpatia hatimiliki.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Zoezi la ugawaji hatimiliki likiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akipanga mti.

 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba akipanda mti.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na wananchi mara baada ya kumaliza kugawa hatimiliki.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na wananchi mara baada ya kumaliza kugawa hatimiliki.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464