Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amesema chama hicho hakijateua wabunge wa viti maalum na hivyo hakuna orodha iliyopelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mnyika amesema leo kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi baada ya wananchama wa chama hicho kuonekana wakiapishwa bungeni kuwa wabunge wa viti maalum.
Mnyika amesema leo kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi baada ya wananchama wa chama hicho kuonekana wakiapishwa bungeni kuwa wabunge wa viti maalum.
Kiongozi huyo katika taarifa yake amesema msimamo wa chama hicho ni ule alioitoa Novemba 8 mwaka huu na kwamba hakuna mabadiliko yoyote.
Taarifa iliyotolewa Novemba 8 inaeleza kuwa “Kamati Kuu Chadema haijafanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum mpaka sasa, hivyo hakuna orodha iliyopelekwa na Katibu Mkuu kwa NEC. Tumedokezwa wanataka kughushi saini na orodha Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye uteuzi haramu na Bunge likabariki.”
Mnyika amesema kuwa wanafuatilia kinachoendelea na wakithibitisha hujuma au usaliti hawatosita kuchukua hatua stahiki.