LICHA YA KICHAPO KUTOKA KWA KMKM, KMC YAAHIDI KUJA KIVINGINE DHIDI YA AZAM FC

 
Wachezaji wa timu za KMC na KMKM wakiwania mpira wakati wa mchezo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo leo na KMC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
 
Na Christina Mwagala, Dar es Salaam
Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imendelea kujifua leo kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Kikosi Maalumu cha kuzuia Magendo Zanzibar KMKM, ikiwa ni katika mikakati ya kujiimarisha kuendelea kwa michezo ya ligi kuu Soka Tanzania Bara Novemba 21 mwaka huu.

Katika mchezo huo, KMKM imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo KMC FC ilipata bao lake kupitia kwa mchezaji wake, Hassan Kapalata.

Aidha mbali na mchezo huo wa leo, KMC FC hadi sasa imeshacheza michezo mitatu ya kirafiki ambayo ni dhidi ya Mbeya kwanza ambapo iliweza kutoka sare ya bila kufungana,Timu ya Benki ya DTB, ambapo KMC FC ili ibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja.

Kupitia michezo hiyo inatoa nafasi kwa walimu kuendelea kukikosa kikosi vizuri na hivyo kufanya marekebisho ili kuhakikisha kwamba katika mchezo dhidi ya Azam Novemba 21 mwaka huu timu hiyo inakwenda kupata matokeo mazuri.

Aidha bado KMC FC ina uwezo mkubwa wakufanya vizuri katika michezo ya ligi kuu inayoanza Jumamosi ijayo kutokana na ubora wa kikosi hicho na kwamba marekebisho mbalimbali yanaendelea kufanywa na walimu na hivyo mashabiki na wapenzi wa Timu hiyo kuweza kupata burudani pamoja na ushindi kwa kila mchezo. 





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464