LICHA YA SARE, YANGA YAPAA KILELENI VPL, YAENDELEZA REKODI YA 'UNBEATEN'


Klabu ya Yanga imekwea mpaka kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, baada ya kutoka suluhu na Gwambina FC, sasa kikosi hicho kimefikisha alama 23, ikiwashusha Azam FC wenye alama 22.
 
Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi kuu Tanzania bara  

Gwanbina FC walikuwa wenyeji wa Yanga SC katika mchezo wa kihistoria ambao timu hizi zilikuwa zinakutana kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu, na mchezo huo umemalizika kwa suluhu (0-0) na kuzifanya timu hizo kugawana alama moja moja.

Yanga wanapata sare ya 2 msimu huu katika michezo 9 na suluhu ya leo inakatisha mwenendo wao wa kushinda michezo 7 mfululizo. Timu hiyo ya wananchi inapanda mpaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo kwa kufikisha alama 23 wanaishusha Azam FC mpka nafasi ya 2 ikiwa na alama 22, kwa matokeo haya Gwambina wanafikisha alama 10 na wanapanda kwa nafasi 2 kutoka nafasi ya 14 mpaka ya 12.

Mchezo Mwingine umechezwa Mkoani Mara katika uwanja wa Karume, ambapo Biashara United walikuwa wakiminyana na timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) na mchezo huo umemalizika kwa sare ya goli 1-1.

Wenyeji Biashara walikuwa wakwanza kupata goli dakika ya 5 kupitia kwa Lenny Kisu, aliyefungwa kwa mkwaju wa penati na KMC walisawazisha goli hilo dakika ya 55 kupitia kwa Lusajo Mwaikenda.

Biashara wanafikisha alama 17 na wanapanda kwa nafasi 1 kutoka nafasi ya 4 mpaka ya 3, KMC FC wanapanda mpaka nafasi ya 5 kutoka ya 6 wakiwa na alama 15. 

CHANZO: EATV 


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464