MWENYEKITI CCM AREJESHA KIWANJA CHA CHAMA ALICHOJIMILIKISHA KWA MIAKA 5


Mkuu wa TAKUKURU mkoani Manyara Holle Makungu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, kata ya Bagamoyo wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Charles Mbaluka, amerejesha kiwanja cha chama hicho alichokuwa amejimilikisha kinyume na utaratibu tangu mwaka 2015.
 
Taarifa hiyo imetolewa hii leo na Mkuu wa TAKUKURU mkoani Manyara Holle Makungu, na kueleza kuwa uchunguzi ulibainika kwamba mwenyekiti huyo kwa kuvunja maadili ya utumishi wa umma na chama chake alijimilikisha eneo hilo kwa kujenga nyumba yake na kuuza kipande kingine cha eneo kwa Sh 700,000. 
 
Hata hivyo mtuhumiwa alikiri kujimilikisha kiwanja hicho kinyume na sheria ambapo kiwanja hicho kitarejeshwa na kukabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Kiteto Kanali Patric Songea, siku itakatayopangwa ili akikabidhi kwa viongozi wa CCM,kata ya Bagamoyo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464