NEC YAPIGILIA MSUMARI SAKATA LA VITI MAALUM CHADEMA

Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt.Wilson Mahera

Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt.Wilson Mahera, amesema kuwa wabunge wanawake wa viti maalum wa CHADEMA waliteuliwa kwa kuzingatia taratibu zote kikatiba na kisheria kupitia orodha ya majina ya wanachama waliopendekezwa iliyowasilishwa na Katibu mkuu wa chama hicho kupitia barua yake.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema kuwa wabunge wanawake wa viti maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) waliteuliwa kwa kuzinagtia taratibu zote za kikatiba na kisheria kupitia orodha iliyowasilishwa na chama hicho.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt.Wilson Mahera Charles, ambayo imeeleza kuwa katibu wa Chadema aliwasilisha orodha ya majina ya wanachama wanaopendekezwa kuteuliwa katika nafasi hiyo katika barua yenye kumb. Na.C/HQ/ADM/20/TU/05/141.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Ndg Stephen Kagaigai (waliokaa) katika picha ya pamoja na Wabunge 19 wa Viti Maalum kutoka CHADEMA mara baada ya kuwaapisha katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Aidha Dkt. Mahera amesema kuwa Tume ilipokea barua ya CHADEMA tarehe 19/11/2020 na kuteua wabunge na madiwani wanawake wa viti maalum kwa kuzingatia matakwa ya katiba na sheria tarehe 20/11/2020

Taarifa hii ya Tume inakuja kufuatia madai ya CHADEMA juu ya wabunge wake waliopishwa bila kufuata taratibu na kanuni za sheria.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464