RAIS MAGUFULI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino mara baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi alipokuwa akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja wa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya hafla fupi ya Uapisho wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi muda mfupi baada ya kumuapisha leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi muda mfupi baada ya kumuapisha leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya hafla fupi ya Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Novemba 2020. PICHA NA IKULU
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464