Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya Miaka 17, wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mchezo wa fainali ya mashindano COSAFA dhidi ya Zambia.
Na Shinyanga Press Club Blog
LEO Novemba 14, 2020 Timu ya Taifa ya Wasichna chini ya umri wa miaka 17 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya soka kwa umri huo kwa mataifa yaliyo kusini mwa Afirika yanayoandaliwa na Shirikisho la vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuibuka na ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Zambia katika mchezo wa fainali uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Bay nchini Afrika Kusini.
Ambapo timu hizo zililazimika kwenda kwenye hatua ya mikwaju ya Penalti baada ya kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90.
Picha za matukio mbalimbali ya uwanjani wakati wa mchezo wa fainali kati ya Tanzania na Zambia.