VSO YAWAWEZESHA VIFAA WAHITIMU VETA SHINYANGA

Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya mapambo na salooni ili kwenda kujiajiri wenyewe.
 
Na Marco Maduhu, Shinyanga
SHIRIKA la Voluntary Services Overseas (VSO), limetoa vifaa kwa wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stad VETA mkoani Shinyanga, ambao walikuwa wakiwafadhili kupata mafunzo chuoni hapo, kwa ajili ya kwenda kujiajiri wenyewe na siyo kutegemea kuajiriwa.

Zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lilifanyika kwenye chuo hicho cha ufundi stad VETA, ambapo wahitimu hao walikuwa wamesomea fani za mapishi, Salooni, Mapambo, Mabomba, Aluminium, umeme, na ufundi pikipiki.

Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, ambao wanajishughulisha na masuala ya kijamii kanda ya ziwa, alisema kuwa wamefadhili mafunzo ya ufundi Stadi vijana 200 kutoka mkoani Shinyanga, ili kuwapatia ujuzi na kuendesha maisha yao.

"Shirika letu baada ya kufadhili vijana hawa mafunzo ya ufundi na kuhitimu, tukaona ni vyema kuwaunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili, na kuwapatia vifaa ambavyo wataanza navyo kujiajiri wenyewe kulingana na fani zao," alisema Katanga.

“Vifaa ambavyo tumetoa ni vya Mapishi, Salooni, ushonaji zikiwamo herehani, ufundi umeme, Aluminium, Mapambo. Mabomba, na pikipiki, ambavyo vijana hawa vitawasaidia kuanzisha shughuli zao na kujipatia kipato, kuliko kurudi nyumbani kukaa kusubili ajira na hatimaye kupoteza ujuzi wao,”aliongeza.

Naye Afisa Vijana kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyang,a Charles Ruchagula, aliwataka vijana hao licha ya kusajili vikundi vyao, wasisite kwenda kuomba mkopo halmashauri fedha za asilimia 10, ambazo Nne kwa vijana zitakazo wasaidia kupanua mitaji yao.

Kwa upande wake Msajili wa Wanafunzi Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoa wa Shinyanga, Rashidi Ntahigiye, aliwataka vijana hao wanapoingia kwenye Soko la kujiajiri wenyewe, wakawe wabunifu kwenye utengenezaji wa bidhaa zao, ili wafanikiwe kupata wateja wengi na kuinuka kiuchumi.

Nao baadhi ya wahitimu hao akiwamo Magreth Zabron aliyesomea fani ya salooni, walishukuru Shirika hilo kuwafadhili mafunzo hayo pamoja na kuwapatia vifaa vya kuanza kazi, na kuahidi kwenda kujituma kuchapa kazi kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao, na hawato waangusha.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa wahitimu wa mafunzo VETA.

Msajili wa wanafunzi chuo cha ufundi stad VETA mkoani Shinyanga Rashidi Ntahigiye, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa wahitimu chuoni hapo waliofadhiliwa mafunzo yao na Shirika la VSO.

Afisa vijana kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Ruchagula, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa wahitimu VETA.

Afisa mtendaji wa Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga Joshua Masengwa, akizungumza kwenye hafla hiyo.

Afisa maendeleo Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga Wema Mashaka, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa wahitimu wa VETA.

Wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stad VETA Mkoani Shinyanga waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.

Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya ushonaji kwa ajili ya kwenda kujiajiri wenyewe.

Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya Aluminium, ili kwenda kujiajiri wenyewe.

Zoezi la kubidhi vifaa likiendelea.

Zoezi la kubidhi vifaa likiendelea , kwa wahitimu wa fani ya mapishi.

Watendaji wa shirika la VSO, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Serikali manispaa ya Shinyanga na chuo cha ufundi stad VETA Mkoani Shinyanga, wakwati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa wahimitu wa fani mbalimbali chuoni hapo. waliofadhiliwa masomo yao na VSO.

Picha ya pamoja wahitimu wa VETA, watendaji wa Shirika la VSO, watumishi wa Serikali na VETA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464