WANAWAKE SHINYANGA WAHAMASISHWA KUJIFUNZA MCHEZO WA NGUMI


Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji Kahama, Lupola Mkomwa akiwanyanua mikono mabondia Issa Salum kutoka Shinyanga na Kudula Tamimu kutoka Morogoro ambao wanatarajia kupambana Katika pambano la gumi za kulipwa kwa Uzito wa kilo 63

Na Salvatory Ntandu, Kahama

Chama cha mchezo wa Ngumi za Ridhaa Tanzania kimewaomba wanawake hususani Mabinti umri wa miaka 18-29 mkoani Shinyanga kujifunza mchezo wa ngumi za ridhaa ikiwa ni mmoja ya njia ya kukabiliana na tatizo la ajira.

Kauli hiyo imetolewa Novemba 2, 2020 na Kaimu Rais wa kamisheni ya mchezo wa ngumi Tanzania, Agapito Basili katika hafla ya kuweka mkataba wa Pambano la ngumi za kulipwa Kati ya Bondia Issa Salumu wa shinyanga na Kudula Tamimu wa mkoani Morogororo litakalofanyika Novemba 28 Mwaka huu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Alisema kuwa mchezo wa ngumi za ridhaa unafaida nyingi hususani ajira kutokana na uwepo wa wanawake wachache kujitokeza kucheza mchezo huo hapa nchini ikilinganishwa na nchi zingine ambazo zinafanya vizuri katika sekta hiyo ya mchezo wa ngumi.

"Tumekuja Kahama kuhamasisha vijana wa kiume na wakike kujifunza mchezo wa ngumi,tumelazimika kuleta pambano kubwa Kati ya Kadula na Issa ili kuhamasisha wadau wa michezo kuupenza mchezo wa ngumi," alisema Basili.

Aliongeza kuwa Kabla ya pambano la Issa na Kudula wa chama hicho kitampandisha ulingoni bondia Mwanamke bingwa wa kimataifa kutoka Tanzania, Oliva Vuja bei ambaye atapambana na Flora Malechela ili kuwahamasisha wanawake mkoani shinyanga kuupenda mchezo huo.

Kwa upande wake Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji Kahama Lupola Mkomwa alisema kuwa ipo haja kwa wadau wa mchezo wa ngumi wilayani humu kujitokeza kuhamasisha vijana kuupenda mchezo huo.

"Wanawake wanaweza kucheza mchezo huu endapo sisi wadau tukishirikiana kwa pamoja kuweka mazingira rafiki yatakayowavutia ili kujikwamua kiuchumi na kujenga afya za miili yao,"alisema Mkomwa

Nae Bondia Issa Salumu ameahidi kumpiga mpinzani wake kutoka mkoani Morogoro Kudula Tamimu ili kuhakikisha anautangaza mkoa wa shinyanga kitaifa na kimataifa katika mchezo wa ngumi za kulipwa.

"Hili ni pambano langu la pili la kitaifa la ngumi za kulipwa Morogoro kwa nilipata ushindi nawaahidi wanashinyanga sitaangushaa,"alisema Issa.

Bondia Kudula Tamimu aliahidi kumpiga mshindani wake Issa kutoka na yeye kuwa na mzoefu katika mapambano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo amecheza na kupata ushindi kwa michezo zaidi ya 10.


Makamu Rais wa Kamisheni ya mchezo wa Ngumi Tanzania, Agapito Basili (kushoto) akiteta jambo na Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji Kahama, Lupola Mkomwa (kulia)

Mabondia Issa Salum (kushto) kutoka Shinyanga na Kudula Tamimu (kulia) kutoka Morogoro ambao wanatarajia kupambana Katika pambano la gumi za kulipwa kwa Uzito wa kilo 63

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464