TVMC YAENDESHA KIKAO KUJADILI HALI YA UKATILI WA KIJINSIA MKOANI SHINYANGA, WANAFUNZI 60 WAPEWA UJAUZITO

 

Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Ngangala akizungumza kwenye kikao cha watoa maamuzi kuanzia ngazi ya Mkoa, halmashauri hadi Kata, kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu - Shinyanga. 
Shirika la The Voice of Margninalized Community (TVMC) la Mkoani Shinyanga limeendesha kikao na watoa maamuzi ngazi ya Mkoa, Halmashauri, na Kata, kujadili hali ya ukatili wa kijinsia, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa huo.


Kikao hicho kimefanyika leo kwenye Hoteli ya Karena Anex na kuhudhuriwa na watoa maamuzi, wakiwemo Wanasheria, Mahakimu, Maofisa Maendeleo ya jamii, Watendaji Kata, Dawati la Polisi, Mratibu wa Ukimwi, na Wadau wa Watoto, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoani Shinyanga Joachim Otaru. 

Mkurugenzi wa Shirika la (TVMC) Mussa Ngangala, akizungumza kwenye kikao hicho, amesema wamekutana na watoa maamuzi hao, kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia pamoja na changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi ili kutokomeza kabisa matukio hayo Mkoani Shinyanga zikiwamo mimba na Ndoa za utotoni. 

“Tumekutana hapa na watoa maamuzi kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri, na Kata, kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia na changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi, pamoja na kutoa mapendekezo ya kwenda kuyafanyia kazi ili kutokomeza ukatili wa kijinsia ndani ya jamii,” amesema Ngangala. 

“Masuala ya ukatili wa kijinsia yana athiri pato la taifa, sababu Serikali inatumia fedha nyingi kwenye mapambano haya, ambayo yanaweza kuzuilika, ili fedha hizo zikatekeleze miradi mingine ya maendeleo, hivyo ni jukumu letu sote tuungane kumaliza matukio haya ya ukatili,”ameongeza. 

Aidha amesema katika tathimini waliyoifanya kwenye Kata Tano, ambazo walikuwa wakitekeleza miradi yao ya kutokomeza ukatili wa kijinsia halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Manispaa, matukio hayo yamepungua kwa asilimia kubwa zikiwamo mimba na ndoa za utotoni ambapo bado kuna changamoto zinahitaji kuwekwa sawa ili kumaliza kabisa ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga. 

Pia amezitaja baadhi ya changamoto ikiwamo ya jamii kumaliza kesi kimya kimya na kuharibu ushahidi, ambayo mwakani wataanza kuifanyia kazi kwa kujenga nyumba salama ya kuhifadhi wahanga wa mimba za utotoni ili kutorudi makwao na kurubuniwa kumkana mtuhumiwa na wazazi wake ambao tayari wameshapewa mali ama mifugo na upande wa mtuhumiwa. 

Kwa upande wake Mgeni Rasmi kwenye kikao hicho Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoani Shinyanga Joachim Otaru, amewataka watendaji hao wa Serikali ambao wanahusika na masuala ya ukatili wa kijinsia, kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na uadilifu mkubwa sambamba na kuwachukulia hatua kali watu ambao bado wanaendeleza masuala hayo ya ukatili. 

Naye Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu mkazi Shinyanga Mary Mrio, amesema jamii bado inahitaji kupewa Elimu ya kutosha juu ya kuacha matukio hayo ya ukatili wa kijinsia pamoja na kuacha kumaliza kesi kimya kimya, na kubainisha kwamba kwa muda mfupi aliofika Shinyanga, kesi nyingi zimefutwa kutokana na kukosa ushahidi. 

Pia Mkuu wa Kituo cha Polisi mjini Shinyanga Grace Salia, ametoa takwimu za matukio ya mimba za utotoni ambazo zilitokea kwenye kipindi cha likizo ya Corona kuwa wanafunzi zaidi ya 60 walipewa ujauzito ambapo baadhi ya kesi zipo Mahakamani na nyingine bado zinaendelea kupelelezwa na amebainishwa kuwa baadhi ya watuhumiwa wa matukio hayo ni ndugu wa karibu na familia.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 

Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Ngangala akizungumza kwenye kikao cha watoa maamuzi kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri hadi Kata, kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Ngangala akizungumza kwenye kikao cha watoa maamuzi kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri hadi Kata, kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoani Shinyanga Joachim Otaru, akizungumza kwenye kikao hicho.

Hakimu mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu mkazi Shinyanga, Mary Mrio, akizungumza kwenye kikao hicho.
Hakimu wa Mahakama ya Samuye Lucy Meshack, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwanasheria wa Serikali mkoani Shinyanga Lightness Tarimo, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga mjini Grace Salia, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mratibu wa tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania Geofrey Mabu, akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Aisha Omary, akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Angle Mwaipopo akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Kahama mji Robert Kwela, akizungumza kwenye kikao hicho.
Watoa maamuzi ngazi ya Mkoa, Halmashauri na Kata wakiwa kwenye kikao cha kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia.
 

Na Marco Maduhu- Shinyanga.


















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464