KATIBU CCM AWASIHI WAHITIMU KIDATO CHA NNE UZOGOLE KUKWEPA VISHAWISHI ILI KUTIMIZA NDOTO ZAO

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga mjini, Aginess Bashemu akizungumza na wananchi na wahitimu wa kidato cha nne shule ya Sekondari Uzogole katika mahafali yao iliyofanyika leo shuleni hapo.

Na Mwandishi Wetu -Shinyanga
Wanafunzi wakike wameshauriwa kuongeza bidii katika masomo ya sayansi ikiwa ni pamoja na kukataa vishawishi wanavyo shawishiwa na wanaume kwa lengo la kuwaharibia ndoto za maisha yao. 

Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga mjini, Aginess Bashemu wakati akizungumza na wahitimu wa kidato cha nne katika shule hiyo ya Sekondari Uzogole iliyopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga alipokuwa mgeni rasmi wa mahafali ya tano ya shule hiyo.

Bashemu amewasa wanafunzi kutotumia simu wakiwa mashuleni na kuwasii kutumia simu hizo kwa kujisomea na kujifunza mbinu mbalimbali za ujasiriamali zitakazo wawezesha kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao. 

Aidha, Katibu huyo ametumia fursa hiyo kuwahimiza vijana wote wilayani humo kuwa wazalendo na kuepuka kutumia simu zao kuichafua serikali hali inayoweza kuwaweka matatani na kuwajibishwa pindi wanapo bainika kuhusika na matumizi mabaya ya mitandao. 

Kwa upande wao wahitimu hao wakisoma risala kupitia mwakilishi wao, Jackline Katambi wameiomba serikali kuwasaidia ukamilishaji wa miundombinu ya vyumba vya madarasa, ili kusaidia kupunguza adha wanazokumbana nazo wanafunzi na walimu katika kutimiza majukumu yao. 
Agnes Bashemu (kulia) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wahitimu aliyefanya vizuri kitaaluma
Mgeni rasmi akikata keki
Vijana wa Skauti katika Shule ya Uzogole wakionyesha umahili wao katika michezo ya viungo
Baadhi ya wananchi na wazazi waliohudhuria mahafali hayo wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani)







Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464