Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakila kiapo
Na Stella Herman, ShinyangaPress Club blog
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wametakiwa kwenda kusimamia fedha za halmashauri zinazotolewa kwa ajaili ya miradi ya wananchi na siyo kugeuza kuwa sehemu ya kujinufaisha wao kwa kutumia fedha hizo kinyume na taratibu.
Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Uongozi wa Umma Kanda ya Tabora, Onesmo Msalangi, ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa madiwani 36 wa halmashauri hiyo baada ya kuapishwa kutumikia nafasi hiyo kwa miaka mitano ijayo.
Alisema madiwani wamechaguliwa kwenda kuwawakilisha wananchi na kusimamia maendeleo na siyo kujinufaisha wao binafsi,kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha mgongano wa maslahi hivyo ni vema wakazingatia sheria ya maadili kwa watumishi wa umma ambayo inawabana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngassa Mboje ambaye ametetea kiti chake kwa mara nyingine kwa kupata kura zote za ndiyo 36 pamoja na Makamu wake Aizack Sengerema alisema ni wakati wa mabadiliko kwa kuhakikisha kuna kuwa na maendeleo makubwa.
Alisema maafisa ugani hawana budi kujipanga kuhakikisha wanatafuta mbegu bora za korosho, miembe na alizeti ili kuwawezesha wakulima kuwa na kilimo chenye tija ikiwa ni pamoja na kuisimamia vizuri idara ya mifugo ili iwanufaishe wafugaji.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza na madiwani aliwataka kila mmoja kwenye eneo lake kwenda kutimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii na kufuatiia miradi yote inayotekelezwa ikiwemo ujenzi wa madarasa,matundu ya vyoo na nyumba za walimu na miundombinu mingine.
Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Uongozi wa Umma Kanda ya Tabora, Onesmo Msalangi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwaapisha madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika kikao hicho
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba akizungumza wakati wa zoezi la kuwaapisha madiwani wa halmashauri hiyo
Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum (CCM) akizungumza katika kikao cha kuwaapisha madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ngassa Mboje
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Izack Sengerema
Madiwani wakila kiapo
Madiwani wakila kiapo