MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WAAPISHWA, WAONYWA KUWA CHANZO CHA MIGOGORO, MBUNGE KATAMBI AWAAHIDI USHIRIKIANO

Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiapa kiapo cha uadilifu na utiii, mara baada ya kumaliza kuapishwa kuwa madiwani Rasmi.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wameapishwa rasmi kuwa madiwani halali, mara baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika Oktoba 28 mwaka huu, huku wakionywa kutokuwa chanzo cha migogoro ndani ya halmashauri hiyo. 

Zoezi la kuapishwa madiwani hao limefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, na kuhudhuliwa pia na Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana na ajira Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini, lililoendeshwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio. 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, akizungumza wakati wa kutoa salamu, amewataka madiwani hao wakafanya kazi kwa ushirikiano na watendaji wote wa Serikali, na wasiwe chanzo na kuibua migogoro bali wakawe watatuzi wa migogoro ndani ya jamii. 

“Nawaomba madiwani mkawe na ushirikiano na viongozi kwenye maeneo yenu, kwa ajili ya kujenga maendeleo ya manispaa ya Shinyanga na kuwatumikia wananchi na msiwe chanzo cha kuibua migogoro,”amesema Mboneko. 

“Pia mkasimamie miradi ya maendeleo, na mapato ya Serikali ili tupate fedha za kuwaletea maendeleo wananchi ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, pamoja na kusimamia asilimia 10 za mikopo ya wanawake, vijana na walemavu, ili tuwainue kiuchumi wananchi wetu,”ameongeza. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana na ajira Patrobasi Katambi, amewataka madiwani hao wakafanye kazi kwa ajili ya maslahi ya wakazi wa Shinyanga na siyo kutanguliza maslahi binafsi, huku akiahidi kutoa ushirikiano kwao, pamoja na viongozi wote na kuomba wamtumie ili wapambane kuleta maendeleo Shinyanga. 

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sinyanga David Nkulila, ameahidi ushirikiano na Madiwani pamoja na watumishi wa Serikali, kwa ajili ya Mstakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo, sambamba na kutatua matatizo ya migogoro mbalimbali, ili mji wa Shinyanga uwe mahali salama pa kuishi. 

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana na ajira Patrobas Katambi, akitoa neno la salam mara baada ya Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kumaliza kuapishwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa neno la Salamu mara baada ya Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kumaliza kuapishwa.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Nchambi, akizungumza kwenye zoezi hilo la uapisho wa madiwani wa Halmashauri ya Mnaispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza mara baada ya kumaliza kuapishwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye zoezi hilo la kuapishwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akiapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio. 
Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Ester Makune akiapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio.
Diwani wa Kata ya Mjini Gulam Mkadamu, ambaye alikuwa Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga kipindi kilichopita akiapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio.
Diwani wa Kata ya Chibe John Kisandu, ambaye alikuwa Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga , akiapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.



Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.

Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Wananchi wa manispaa ya Shinyanga wakishuhudia uapisho wa madiwani wa Halmashauri hiyo.
Wananchi wakiendelea kushuhudia zoezi la uapisho wa madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.
Wananachi na viongozi mbalimbali wa Serikali wakishuhudia zoezi hilo la Uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.
Viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini, akishuhudia zoezi la uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la uapisho madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea kushuhudiwa.
Zoezi la uapisho madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea kushuhudiwa.

Zoezi la uapisho madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea kushuhudiwa.
Zoezi la uapisho madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea kushuhudiwa.
Pongezi zikitawala mara baada ya madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kumaliza kuapishwa.
Furaha zikitawala mara baada ya madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kumaliza kuapishwa.
Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, wakiingia ukumbini kuendelea na Baraza mara baada ya kumaliza kuapishwa.
Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, wakiingia ukumbini kuendelea na Baraza mara baada ya kumaliza kuapishwa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, wakwanza, akielekea kwenye ukumbi kwa ajili ya kuanza Baraza la Madiwani mara baada ya kumaliza kuapishwa, katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Nchi ya Waziri mkuu kazi, vijana, na ajira, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, akifuatiwa na Naibu Meya Ester Makune.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, wapili kutoka kushoto, akifungua Baraza la Madiwani.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.


















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464