MAKAMU WA RAIS ATAJA VIGEZO VILIVYOTAZAMWA UTEUZI MAWAZIRI 21 NA MANAIBU 22 WALIOAPISHWA LEO, NDUGAI AWATAKA KUTOKWEPA VIKAO VYA BUNGE, KAMATI ZAKE

Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Na Damian Masyenene
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli leo Desemba 9, 2020 amewaapisha Mawaziri 21 na Manaibu Waziri 23 aliowateua hivi karibuni, ambapo hafla hiyo imefanyika Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

Akitoa salamu kwa viongozi hao, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amemshukuru Rais kwa kuandaa safu hiyo kwa umakini mkubwa sana, ambapo mawaziri wenyeji 13 walifanya kazi nzuri ambayo imewafanya waaminiwe tena, huku wapya wakiwa 10 na watano kati yao walikuwa makatibu wakuu, wanne walikuwa manaibu waziri, mmoja katoka kamati ya bajeti ya Bunge.

Amesema kati ya Manaibu Waziri 22 walioapa, sita tu ndiyo wenyeji na wapya ni 17, huku akibainisha kuwa kupata safu hiyo kuna mambo mengi yameangaliwa yakiwemo ya kitaaluma, uwajibikaji katika maeneo ya kazi, uwajibikaji kisiasa na maisha yao ndani ya jamii ikiwemo mienendo ya maisha, tumeona tuanze na safu hii kwakuwa tunayo safu nyinyine ya akiba (reserve).

"Tunamhukuru Rais kwa kutunyoosha kwa miaka mitano, na katika mawaziri mlioapa leo wapo ambao tulinyooshwa pamoja, na hawa wapya inabidi tuwasaidie ili twende nao pamoja....kazi tuliyofanya kwenye kipindi kilichopita ndiyo imeleta matunda haya kwenye uchaguzi

"Tunapoingia maofisini madaraka haya tuliyokabidhiwa siyo ya kwetu, ni madaraka na utumishi wa wnaanchi, matumaini yetu kwenu mtaenda kufanya kazi kileo kwa kasi zaidi kuwatrumikia watanzania. 

"Mategemeo yetu ni kwamba hatutakwenda kufamnya lolote ila kuwatumikia watanzania kwa utumishi uliotukuka, matumaini ya wananchi ni makubwa, shida za wananchi bado ni nyingi, tukawatumikie wananchi tutoe majawabu kwa shida zinazowasumbua wananchi," amesema.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amemshukuru Rais kwa kuwateua mawaziri hao na kuonyesha imani kubwa aliyonao kwao, huku akiwapongeza mawaaziri wenzake kwa kuaminiwa.

"Tuna jukumu la kuwatumikia watanzania, serikali hii imejipambanua kuwa ni ya kusema na kutenda. Katika kipindi cha miaka mitano tumefanya mabadiliko makubwa sana ya maadili ya watumishi wa umma.

"Na timu hii ya mawaziri ni ya kufanya kazi, twende tukachape kazi, Tunakwenda kufanya kazi kwa bidii na kumshauri Rais wetu," amesema.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amewataka wateuliwa hao kufanya kazi ambayo siku wakiondoka waache alama na kumbukumbu kwa watanzania.

"Mheshimiwa Rais alizunguka maeneo mengi ya nchi hii kwenye kampeni, amebeba mzito mzito sana wa Wataznania, nendeni mkamsaidie, msiende kulewa madaraka ya uwaziri kumbukeni nyinyi na watumishi, tusaidieni ifikapo 2025 tuone Tanzania ina mabadiliko makubwa sana.

"Ni muhimu kwelikweli kuhudhuria vikao vya bunge na kamati za bunge ni wajibu wa kikatiba, kule ndipo mnapokutana na wawakilishi wa wananchi na matatizo yao," amesisitiza.

Naye Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Issa Juma akitoa salamu kwa mawaziri na manaibu waziri walioapishwa leo, amewakumbusha viongozi walioteuliwa kuwa wana mzigo mzito sana wa matumaini kutoka kwa wananchi na kutimiza dira ya taifa ya mawendeleo iliyozinduliwa na Rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa inayohitimishwa 2025, huku akiwaahidi kuwa mahakama itawapa ushirikiano.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464