UDIDA WATOA MSAADA WA MIFUKO YA SARUJI KUKARABATI VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA SEKONDARI TOWN



Mkurugenzi wa Shirika la UDIDA Jasson Kyaruzi, kulia akimkabidhi mifuko ya Saruji Mkuu wa Shule ya Sekondari Town Jasson Regasira.

Na Marco Maduhu Shinyanga

Shirika la UDIDA ambalo linajishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii mkoani Shinyanga limetoa msaada wa mifuko ya Saruji 15 katika shule ya Sekondari Town iliyopo manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kukarabati vyumba vya madarasa shuleni hapo. 

Mkurugenzi wa Shirika hilo Jasson Kyaruzi akizungumza jana wakati wa kukabidhi mifuko hiyo ya Saruji, alisema wanaunga mkono juhudi za Serikali kwa kutatua changamoto ya uchakavu na upungufu wa vyumba vya madarasa. 

Alisema msaada huo wa mifuko ya saruji 15 ni mwanzo, ambapo wataendelea kujitoa zaidi ili kukakikisha wanashirikiana na Serikali kukarabati miundombinu ya shule, kwa ajili ya kuwajengea mazingira mazuri wanafunzi ya kusoma na kupata ufaulu mzuri ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa. 

“Shirika letu la UDIDA tumeguswa na changamoto ya uchakavu na upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule hii ya Sekondari ya Town, ambayo ipo jirani na ofisi zetu, ndipo tukaamua tutoe mchango wetu wa mifuko 15 ya Saruji, ilikusaidiana na Serikali kutatua changamoto hii,”alisema Kyaruzi. 

Kwa upande wake mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari Town Jasson Regasira, alishukuru msaada huo wa mifuko ya Saruji, na kusema imefika katika wakati muafaka kutokana na sasa wapo kwenye ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo. 

Alisema Shule hiyo inakabiliwa na uchakavu wa vyumba vya madarasa, pamoja na upungufu wa vyumba Vinne, vilivyopo ni 12 na mahitaji ni 16, ambapo kwa sasa wanajenga vyumba vitatu na kuendelea kukabiliwa na uhaba wa chumba kimoja. 

Aidha Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Masovela, akitangaza matokeo ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani mkoani humo ni 26,382, na ambao wamebaki kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa ni 234. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Shirika la UDIDA Jasson Kyaruzi, akizungumza kabla ya kukabidhi mifuko 15 ya Saruji shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Town Jasson Regasira, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mifuko hiyo ya Saruji.
Baadhi ya walimu katika shule hiyo ya Sekondari Town wakiwa kwenye zoezi la kukabidhiwa mifuko ya Saruji.

Walimu wakiwa kwenye makabidhiano ya mifuko ya Saruji.

Wana UDIDA wakiwa kwenye ofisi za walimu katika shule ya Sekondari Town kwa ajili ya kukabidhi mifuko 15 ya Saruji.
Mkurugenzi wa Shirika la UDIDA Jasson Kyaruzi, kulia akimkabidhi mifuko ya Saruji Mkuu wa Shule ya Sekondari Town Jasson Regasira.
Mkurugenzi wa Shirika la UDIDA Jasson Kyaruzi, akiwasihi wanafunzi katika shule hiyo ya Sekondari Town wasome kwa bidii.
Awali wanafunzi wakishusha mifuko hiyo ya Saruji.
Wanafunzi wakiingiza ndani ya ofisi mifuko hiyo ya Saruji.

Wanafunzi wakiingiza ndani ya ofisi mifuko hiyo ya Saruji.














































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464