Waziri wa Nishati Dkr Medard Kalemani, akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Mgodi wa Nyangalata na kuwa hakikishia kuwa Serikali itawaletea umeme ili kuwapunguzia gharama kubwa za uzalishaji madini kwa njia ya mafuta mazito na Jenereta.
Na Marco Maduhu, Kahama
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga, ambapo leo ametembelea Mgodi mdogo wa uchimbaji madini ya dhahabu Nyangalata uliopo Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama.
Akiwa katika mgodi huo akiwa ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Msalala, Iddi Kasimu (CCM), Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha na maofisa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), amesema Serikali inataka kasi ya usambazaji umeme kwenye migodi midogo ya madini ili kuondoa gharama kubwa za uzalishaji wa madini hayo.
Amesema kwenye migodi midogo ya uchimbaji wa madini ya dhahabu, hua wanatumia gharama kubwa ya uzalishaji wa madini hayo kutokana na kutumia mafuta mazito ama Jenereta, lakini wakitumia Nishati ya umeme kutoka Gridi ya Taifa hawatakuwa wakiingia kwenye gharama hizo kubwa kama ilivyo sasa.
“Rais John Magufuli ameshatoa fedha ili wananchi wasambaziwe huduma ya umeme yakiwamo na maeneo ya migodi midogo, hivyo naagiza Januari 3, 2021, watu wa Survey wawe wameshafika kwenye eneo hili la mgodi wa Nyangalata na kuanza mchakato wa kuleta huduma hapa ya umeme, pamoja na kwenye mgodi wa Tambarare,” amesema Kalemani.
“Lengo la Rais ni kuwakuza wachimbaji wadogo, ili wachimbe madini kwa ufanisi, na kuongeza kasi ya uzalishaji wa madini na kupata mapato mengi, na hatimaye kukua kiuchumi na taifa kwa ujumla, na mkitumia umeme mtaokoa gharama ya asilimia 80 ya uzalishaji madini ambayo mnaingia kwa sasa na kutumia Shilingi Milioni 800 kwa mwezi,”ameongeza.
Pia amesema Serikali hadi kufikia Februari 5, 2021, wanatarajia kuanza kusambaza pia huduma ya nishati ya umeme kwenye vitongoji na vijiji vyote nchi nzima, ambapo katika wilaya hiyo ya Kahama vimesalia vijiji 147 na Halmashauri ya Msalala kuna vijiji 60 tu.
Katika hatua Nyingine Waziri Kalemani, akiwa katika kituo cha kupokea, kusambaza na kupoza umeme (Sub station) kilichopo Bulyanhuru wilayani Kahama, ambacho kinapokea umeme kutoka Ibadakuli mjini Shinyanga, amekazia suala kutaka umeme hovyo hasa katika siku kuu ya Mwaka Mpya, na kuonya umeme huo usije ukathubutu kukatika hata kidogo Mkoani Geita wala kushitua, ambapo kwa sasa Rais yupo kwenye mapumziko ya sikuu hiyo nyumbani kwake Chato.
Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu, amesema kasi hiyo ya usambazaji umeme kwenye makazi ya watu na maeneo ya migodi, itakuwa ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa maendeleo kwa wananchi pamoja na wachimbaji wadogo, ikiwamo na kufungua vitega uchumi vya umeme na kuwaongezea kipato.
Kwa upande wake mmoja wa wachimbaji wadogo kutoka mgodi huo wa Nyangalata Alex Manyama, amesema kutokana na kutumia mafuta mazito kuzalisha madini hayo, amekuwa wakitumia kwa siku kiasi cha Sh. 900,000, huku akiiomba Serikali iwapelekee nishati ya umeme ili kuwapunguzia matumizi hayo ya gharama kubwa.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza kwenye kituo cha kupokea, kusambaza na kupoza umeme kilichopo eneo la Bulyanhulu wilayani Kahama. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Msalala, Iddi Kasimu.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kasimu akizungumza na wachimbaji wadogo Nyangalata.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga, akizungumza na wachimbaji wadogo wa Nyangalata.
Wachimbaji wadogo wa madini Nyangalata wakiwa kwenye mkutano wa Waziri wa Nishati Dkr Medard Kalemani.
Wachimbaji wadogo wa madini Nyangalata wakiwa kwenye mkutano wa Waziri wa Nishati Dkr Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati Dkr Medard Kalemani, akiangalia namna ya uzalishaji madini ya dhahabu kwa wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Nyangalata, kwa kutumia Jenereta ambapo wanaingia gharama kubwa.
Waziri wa Nishati Dkr Medard Kalemani, kushoto, akisikiliza maelezo kwa mchimbaji mdogo Alex Manyama namna wanavyotumia gharama kubwa kuzalisha madini ya dhahabu kwa njia ya mafuta mazito au Jenereta.
Waziri wa Nishati Dkr Medard Kaleman, akizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhuru wilayani Kahama, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu
Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu, akizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhuru wilayani Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Annamringfi Macha kizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhuru.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga, kizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhuru.
Waziri wa Nishati Dkr Medard Kalemani, akisililiza maelezo kutoka kwa msimamizi wa kituo cha kupokea umeme, kusambaza na kupoza kutoka eneo la Bulyanhuru Amos Asheli.
Awali Waziri wa Nishat Dkr Medard Kalemani, akiwa kwenye ziara katika mgodi wa madini Nyangalata.
Ziara ikiendelea.
Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhuru.
Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhuru.
Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhulu.